Zlatan Ibrahimovic Ajengewa Sanamu La Heshima Nchini Sweden

9th October 2019

MALMO, Swededn -Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amepewa heshima ya kujengewa sanamu na Shirikisho la Soka Nchini Sweden kutokana na mchango wake mkubwa kwenye soka la nchi hiyo.

Zlatan Ibrahimovic
Zlatan Ibrahimovic
SUMMARY

Baadhi ya wachezaji wengine ambao nao wamepata heshima ya kujengewa masanamu ni pamoja na Cristiano Ronaldo, David Beckham na Mohamed Salah.

Sanamu hilo limezinduliwa jana nje ya uwanja wa timu ya soka ya Malmo mahala ambapo nyota huyo alianza maisha yake ya soka huku mamia ya mashabiki wa soka wakipata nafasi ya kuhudhuria.

Ibrahimovic, 38, amecheza timu ya taifa ya Sweden kwa jumla ya michezo 116 na kufunga mabao 62 kuanza mwaka 2001 hadi 2016.

Mbali na Malmo, Ibrahimovic pia alicheza timu za Ajax, Juventus, Inter Milan, Barcelona, AC Milan, PSG na LA Galaxy aliyojiunga nayo mwaka 2018 akitokea Manchester United.

Baadhi ya wachezaji wengine ambao nao wamepata heshima ya kujengewa masanamu ni pamoja na Cristiano Ronaldo, David Beckham na Mohamed Salah.

"Haijalishi umetoka wapi au upo wapi kwa sasa au nini unapenda, lakini sanamu ni ishara tosha ya kwamba hakuna kitu kinachoshindikana," amesema Ibrahimovic.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya