Dokezo: Maisha Ya Unai Emery Ndani Ya Arsenal Kwenye Namba

1st December 2019

LONDON, Uingereza- Baada ya Unai Emery kutimuliwa na Arsenal SportPesa News inakuletea dokezo ambalo linaonesha maisha yake kwa ujumla yakiwa ndani ya namba kwa kipindi cha miezi 18 aliyoishi London.

Unai Emery
Unai Emery
SUMMARY

9- Idadi ya wachezaji makinda U20 ambao wamepata nafasi ya kucheza Arsenal kwenye kipindi cha Unai madarakani

3- Ni idadi ya mechi alizoshinda dhidi ya timu kubwa za Uingereza ama kwa jina lingine unaweza kuziita 'Top Six"

7- Hii ni idadi ya mechi saba mfululizo ambazo hajashinda tangu mwezi Oktoba hadi Novemba, 2019 na mwisho hadi kutimuliwa.

8- Hii ni idadi ya mechi alizoshinda ugenini kwenye mechi za ligi kuu ya Uingereza tangu alipopewa timu, kati ya mechi hizo nane ni moja tu ndiyo aliyoshinda msimu huu.

9- Idadi ya wachezaji makinda U20 ambao wamepata nafasi ya kucheza Arsenal kwenye kipindi cha Unai madarakani

15- Hii ni idadi ya maboko ambayo yamefanywa na wachezaji wake na kupelekea timu pinzani kunufaika kwa kufunga mabao. Idadi hii ni kubwa kuliko timu nyingine yeyote kwenye EPL Kwa kipindi hicho ambacho Emery alikuwa kocha wa Arsenal.

19- Hii ni idadi ya alama ambazo wamepoteza Arsenal wakati wakiwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda mchezo na kuzoa alama zote tatu.

22- Idadi ya mechi ambazo Arsenal walicheza mfululizo bila kufungwa kati ya Agosti hadi Desemba, 2018. Kipindi hiki Arsenal walikuwa wa moto balaa

42.1- Hii ni asilimia ya mabao ambayo yamefungwa na washambuliaji wawili Aubameyang na Lacazette chini ya Unai. Wamefunga mabao 64 kati ya 152 yaliyofungwa kwa ujumla.

55.1- Asilimia ya ushindi kwa michezo yote aliyosimamia Unai akiwa kama kocha wa Arsenal. Mtangulizi wake Arsene Wenger alikuwa na asilimia 57.2 ya ushindi kwenye michezo 1235.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya