Spurs Ya Mourinho Yazidi Kuchuma Pointi EPL, Liverpool Hawafungiki

1st December 2019

LONDON, Uingereza- Kocha Jose Mourinho ameiongoza Tottenham Hotspurs kwenye ushindi wa tatu mfululizo kwenye michuano yote baada ya kuwafunga Bournemouth kwa mabao 3-2 kwenye mchezo uliofanyika nyumbani White Hart Lane.

Dele Ali
Dele Ali
SUMMARY

Ushindi huo umewasogeza Spurs hadi kwenye nafasi ya tano kwenye msimamo wakiwa na alama 20 baada ya kushuka dimbani mara 14.

Delle Alli ambaye ni kama nyota aliyezaliwa upya ndani ya kikosi hicho ndiyo aliyeongoza mauaji akifunga mabao mawili huku bao moja likifungwa na Mousa Sissoko.

Harry Wilson aliyetokea benchi kwa upande wa Bournemouth alifunga mabao mawili dakika za mwisho ambayo yalibadilisha sura ya mchezo na bado nusu yatibue mood ya mashabiki wa Spurs ambao kwa muda mrefu walikuwa wakiimba nyimbo za kumsifu kocha Mourinho.

Ushindi huo umewasogeza Spurs hadi kwenye nafasi ya tano kwenye msimamo wakiwa na alama 20 baada ya kushuka dimbani mara 14.

Van Dijk Aokoa Jahazi

Baada ya kufanya kazi ya kuzuia, mlinzi wa kati wa Liverpool, Virgil van Dijk amegeuka mshambuliaji kwa muda akifunga mabao mawili ya kichwa na kuipa timu yake ushindi wa 2-1 dhidi ya Brighton.

Bao la Brighton nalo limefungwa na mlinzi wa kati Lewis Dunk. Matokeo hayo yanawafanya Liverpool kuzidi kujikita kileleni huku wakiwa ndiyo timu pekee ambayo haijafungwa hadi sasa kwenye michezo 14.

Kwenye mchezo huo tumeshuhudia mlinda lango wa Liverpool, Alisson akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kudaka mpira nje ya eneo la boksi.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya