La Liga: Sergio Ramos Aipeleka Real Madrid Kileleni Kwa Kuifunga Alaves

1st December 2019

MADRID, Hispania- Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos amefunga bao moja ambalo limeiwezesha timu yake ya kuibuka na ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Alaves.

Sergio Ramos
Sergio Ramos
SUMMARY

Ramos alianza kuwafungia bao Madrid kwa kichwa mapema kipindi cha pili lakini bao hilo lilidumu kwa dakika 10 tu kabla ya wenyeji kuchomoa kupitita Lucas Perez aliyefunga kwa mkwaju wa penati.

Ushindi huo umeipeleka Real Madrid kileleni japo kwa muda na watashuka endapo Barcelona watafanikiwa kuwafunga Atletico Madrid.

Ramos alianza kuwafungia bao Madrid kwa kichwa mapema kipindi cha pili lakini bao hilo lilidumu kwa dakika 10 tu kabla ya wenyeji kuchomoa kupitita Lucas Perez aliyefunga kwa mkwaju wa penati.

Dani Carvajal aliongeza bao la pili kwa Madrid dakika tatu baada ya Alaves kuchomoa na bao hilo lilidumu hadi mwisho wa mchezo.

Kwenye mchezo huo winga Gareth Bale alipatwa nafasi ya kuanzishwa kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza tangu kocha Zinedin Zidane alipomuanzisha kwa mara ya mwisho Oktoba 5.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya