Euro 2020: Hatumwi Mtoto Dukani Kundi F: Ureno, Ujerumani, Ufaransa Uso Kwa Uso

1st December 2019

NYON, Uswiz- Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Ulaya, EUFA wameweka hadharani makundi kwa ajili y michuano ya Euro 2020 ambapo mabingwa wa dunia Ufaransa wamejikuta ndani ya kundi moja la F dhidi ya mabingwa wa ulaya Ureno.

Euro 2020
Euro 2020
SUMMARY

Kweye mechi za kundi hilo tutapata fursa ya kuona jinsi nyota wakubwa duniani kama vile Cristiano Ronaldo, Paul Pogba, Antoine Griezmann wakipepetana wenyewe kwa wenyewe na mwisho wa siku timu mbili kutoka kila kundi ndiyo zitahitajika kwenye hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ambayo inatarajia kuanza Juni mwakani.

Kundi hilo pia linawajumuisha Ujerumani ambao ni mabingwa wa dunia mwaka 2014 huku timu ya nne ikiwa bado haijajulikana ndani ya kundi hilo hadi pale michezo ya play offs itakapochezwa.

Kweye mechi za kundi hilo tutapata fursa ya kuona jinsi nyota wakubwa duniani kama vile Cristiano Ronaldo, Paul Pogba, Antoine Griezmann wakipepetana wenyewe kwa wenyewe na mwisho wa siku timu mbili kutoka kila kundi ndiyo zitahitajika kwenye hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ambayo inatarajia kuanza Juni mwakani.

Makundi ya B, C, D, E na F bado hayajakamilika yakisubiri timu moja kila mmoja ambazo zitatokana na mechi za mchujo (Play Offs).

Makundi Kamili

Kundi A: Italy, Switzerland, Turkey, Wales

Kundi B: Belgium, Russia, Denmark, Finland

Kundi C: Ukraine, Netherlands, Austria, Kutoka Play Offs

Kundi D: England, Croatia, Czech Republic, Kutoka Play Offs

Kundi E: Spain, Poland, Sweden, Kutoka Play Offs

Kundi F: Germany, France, Portugal, Kutoka Play Offs

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya