Yaliyojiri Tennis: Novak Djockovi, Dominic Thiem Waendeleza Undava Shanghai Masters

10th October 2019

SHANGHAI, China- Baada ya ushindi wa kishindo kwenye michuano ya Japan Open, Novak Djokovic ameendeleza moto wake kwenye michuano ya Shanghai Masters baada ya kumfunga Denis Shapovalov.

Novak Djokovic
Novak Djokovic
SUMMARY

Kwenye michuano ya Tianjin Open, mwana dada Heather Watson amepata ushindi wake mkubwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili akimfurumusha Mchina, Wang Qiang kwa jumla ya seti 6-3 6-0.

Djokovic ameibuka na ushindi wa seti 6-3 6-3 na sasa atakutana na bingwa mtetezi wa michuano hiyo Mmarekani, John Isner kwenye hatua inayofuata.

Isner kwa upande wake amemfunga Mfaransa, Lucas Pouille kwa jumla ya seti 7-5 6-3.

Naye bingwa wa michuano ya China Open, Dominic Thiem amefanikiwa kumlaza Mhispania, Pablo Busta kwa jumla ya seti 7-6 (7-3) 6-3 na kufanikiwa kutinga katika mzunguko wa tatu wa michuano hiyo.

Kwenye michuano ya Tianjin Open, mwana dada Heather Watson amepata ushindi wake mkubwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili akimfurumusha Mchina, Wang Qiang kwa jumla ya seti 6-3 6-0.

Kwa ushindi huo, mwana dada huyo wa Uingereza atacheza dhidi ya Mpoland, Magda Linette au Mjapan Kurumi Nara ambao watacheza hapo baadaye.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya