Yaliyojiri NBA: James Harden Aipaisha Rockets, GSW, LA Clippers, Raptors Zatakata

29th October 2019

OKLAHOMA, Marekani- James Harden alikuwa kwenye kiwango bora alfajiri ya leo wakati akifunga vikapu 40 na kuisaidia timu yake ya Houston Rockets kuibuka na ushindi wa 112-116 dhidi ya wenyeji Oklahoma City Thunder.

James Harden
James Harden
SUMMARY

Stephen Curry alikuwa muhimili muhimu ndani ya Warriors akifunga vikapu 26 huku Draymond Green naye akiongoza vingine 16 kwa mabingwa hao mara tano mfululizo wa Kanda Ya Magharibi.

Huo ni ushindi wa pili kwa Rockets ndani ya mechi tatu ambazo wameshuka dimbani hadi hivi asasa. Wakali hao walianza ligi vibaya baada ya kupigwa kwenye mchezo wao wa kwanza tu dhidi ya Mulwaukee Bucks.

Mbali na Harden lakini pia alama 38 zilizofungwa na Russell Westbrook na PJ Tucker kwa pamoja zilikuwa na umuhimu mkubwa katika kupelekea matokeo ya ushindi kwa Rockets.

Dennis Scroder na Gilgeous Alexader wamefunga vikapu 22 kila mmoja kwa upande wa Thunder lakini matokeo ya ushindi hayakuweza kwenda upande wao.

LA Clippers Waamka Tena

Baada ya kujikwaa kwenye mechi iliyopita, LA Clippers wameamka na sasa wanaendelea na safari baada ya ushindi wa 96-111 dhidi ya Charlotte Hornets.

Kama kawaida staa wao Kawhi Leonard amefanikisha ushindi huo akifunga vikapu 30 ambavyo ni vingi ukilinganisha na wachezaji wengine kwenye mchezo huo.

GSW Wameanza Ligi?

Baada ya kuanza na vichapo viwili mfululizo kwenye mechi zao mbili za awali, kwa mara ya kwanza Golden State Warriors wameonja ladha ya ushindi msimu huu.

Hiyo ni baada ya kuwafunga New Orleans Pelicans kwa jumla ya vikapu 134-123.

Stephen Curry alikuwa muhimili muhimu ndani ya Warriors akifunga vikapu 26 huku Draymond Green naye akiongoza vingine 16 kwa mabingwa hao mara tano mfululizo wa Kanda Ya Magharibi.

Matokeo Kamili

Oklahoma City Thunder 112-116 Houston Rockets

Charlotte Hornets 96-111 LA Clippers

Golden State Warriors 134-123 New Orleans Pelicans

Philadelphia 76ers 105-103 Atlanta Hawks

Portland Trail Blazers 110-113 San Antonio Spurs

Cleveland Cavaliers 112-129 Milwaukee Bucks

Denver Nuggets 101-94 Sacramento Kings

Utah Jazz 96-95 Phoenix Suns (OT)

Orlando Magic 95-104 Toronto Raptors

Indiana Pacers 94-96 Detroit Pistons

Chicago Bulls 98-105 New York Knicks

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya