WTA: Majeraha Ya Bega Yamuondoa Naomi Osaka Kwenye Mashindano Ya Dunia

29th October 2019

SHENZHEN, China- Mchezaji wa tenesi mwana dada Naomi Osaka amejiondoa kwenye mashindano ya Dunia yanayofanyika China kufuatia maumivu aliyopata kweye bega lake.

Naomi Osaka
Naomi Osaka
SUMMARY

Kwa maana hiyo sasa Kiki Betenes anatarajiwa kuchukuwa nafasi ya Osaka ambaye alikuwa kwenye kundi lililopewa jina "Red Group".

Osaka, 22 ambaye siku ya Jumapili alimfunga Petra Kvitova leo alikuwa anatarajia kukutana na mchezaji wa tenesi namba moja kwa ubora upande wa wanawake Ashleigh Barty lakini taarifa iliyotiolewa na kambi ya Mjapan huyo ni kwamba hatoweza kucheza mchezo huo.

Kwa maana hiyo sasa Kiki Betenes anatarajiwa kuchukuwa nafasi ya Osaka ambaye alikuwa kwenye kundi lililopewa jina "Red Group".

Mshindano ya WTA yanashirikisha wachezaji 8 kwa ubora duniani ambapo wanagawanywa kwenye makundi mawili na washindi wa nafasi ya kwanza na ya pili wanasonga mbele kufika kwenye hatua ya nusu fainali.

Kwa upande wa wanaume, Rogder Federer naye amejitoa kwenye mashindano ya Paris Masters kwa madai ya kutafuta muda zaidi wa kujiandaa na mashindano ya ATP yanayotarajiwa kufanyika London, Uingereza kuanzia Novemba 2.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya