Usiku Wa Vitasa: Mwakinyo Kumaliza Ubishi Mbele Ya Mfilipino Leo?

29th November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Leo ndiyo leo asemaye kesho muongo! siku ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na Watanzania wote duniani kutaka kumshuhudia kijana wakitanzania Hassan Mwakinyo akitupa masumbwi dhidi ya Mphilipino, Arnel Tinampay imefika.

Hassan Mwakinyo
Hassan Mwakinyo
SUMMARY

Ushindi wake wa KO raundi ya pili ugenini dhidi ya Muingereza, Sam Egginnton mnamo Septemba mwaka jana ndani ya mji wa Birmingham unabaki kuwa kielelezo tosha cha ubora wa Mwakinyo hadi sasa.

Ni siku ya machozi, jasho na damu naweza kuuita hivyo ambapo Watanzania watakuwa na fursa adimu ya kulishuhudia pambano la kimataifa baina ya mabondia hao nyota ambao watazichapa kwa raundi  10.

Kila mmoja amejinasibu kumteketeza mwenzake kabla hata ya raundi 10 kutimia lakini kama watanzania leo tutakuwa nyuma ya ndugu yetu Mwakinyo ambaye pia ni balozi wa kampuni bora kabisa ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa.

Ipi Nafasi Ya Mabondia Hao

Licha ya kuwa Mwakinyo hana uzoefu mkubwa kumzidi Tinampay lakini ubora wake ulingoni unaweza kuwa faida kubwa kwake kwa siku ya leo.

Mwakinyo ambaye kwasasa anatajawa kuwa ni bondia namba moja kwa ubora kwa wenye uzito wa kati Afrika ana sifika zaidi kwa kurusha makombora mazito na spidi ya cherehani.

Ndani ya uzoefu wake wa miaka minne tu ndani ya masumbwi ya kulipwa lakini Mwakinyo ameshafanya mabalaa ambayo yamewaacha watu vinywa wazi hadi kufikia sasa.


Ushindi wake wa KO raundi ya pili ugenini dhidi ya Muingereza, Sam Egginnton mnamo Septemba mwaka jana ndani ya mji wa Birmingham unabaki kuwa kielelezo tosha cha ubora wa Mwakinyo hadi sasa.

Leo anakutana na Tinampay ambaye ana uzoefu wa miaka 16 ndani ya ulingo wa masumbwi ya kulipwa. Bondia huyu wakati fulani alikuwa akifanya mazoezi na bingwa wa dunia Manny Pacquiao na kitu hicho kimfanya kuwa moto kwa kiasi fulani.

Kuonesha kwamba Tinampay amelipania sana pambano hili alitua nchini tangu Jumatatu ya wiki iliyopita ambapo alikuja na wapishi wake pamoja na wasaidizi mbalimbali kwa ajili ya kuweka kambi ya hapa Tanzania.

Mapambano Ya Utangulizi

Kabla ya pambano la Mwakinyo dhidi ya Tinampay kutakuwa na mapambano sita ya utangulizi kwa mujibu wa promota J Msangi.

Hata hivyo pambano ambalo linaonekana kuteka hisia za watu ni lile ambalo litamkutanisha Rais wa Mabibo, Mfaume Mfaume ambaye atazichapa uso kwa uso na Keis Ally.

Pambano hilo linatarajia kuvuta hisia za watu wengi kwani shamra shamra zake zimeanza tangu jana ambapo umati wa mashabiki wa mabondia hao ulijitokeza wakati wa shughuli za kupima uzito.

Na leo kunatarajiwa kuwa na mafuriko makubwa kabisa ya mashabiki kutoka katika viunga vya maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Ratiba Kamili Utangulizi

Mohamed Bakari vs Said Chino (Feather Raundi 8)

Adam Yusuph Lazaro vs Meshack Mwankemwa 

Twaha Kiduku vs France Ramabolu (Afrika Kusini)

Loren Japhet vs Salim Mjengo (Super Bantam. Raundi 8)

Mfaume Mfaume vs Keis Ally (Super Welter. Raundi 8)

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya