Uingereza Watinga Nusu Fainali Kombe La Dunia La Rugby

20th October 2019

YOKOHAMA, Japan- Timu ya taifa ya Uingereza mchezo wa Rugby wamefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia baada ya kuibuka na ushindi wa 40-16 dhidi ya Australia.

England
England
SUMMARY

Hata hivyo Uingereza watakuwa na kazi ya ziada dhidi ya New Zealand ambao wamekuwa ni wababe wa mchezo huo kwa miaka ya hivi karibuni wakishinda kombe la dunia mara mbili mfululizo 2007, 2015.

Kwa matokeo hayo, Uingereza sasa watakutana na wababe New Zealand kwenye mchezo wa nusu fainali ambao umepangwa kuchezwa Jumamosi ijayo jijini Yokohama.

Kukosekana kwa George Ford kwenye kikosi cha wachezaji 15 wa awali ilikuwa ni mada kubwa wakati wa kuelekea mchezo huo.

Hata hivyo jina la nahodha wa Uingereza, Owen Farrell ambaye alikuwa na hatihati ya kucheza mchezo lilionekana na kuleta faraja kidogo kwa mashabiki wa Uingereza.

Nahodha huyo hakuwaangusha mashabiki wao baada ya kufanikiwa kufunnga alama 16 ambazo ni nyingi kuwahi kufungwa na mchezaji mmoja kwenye kombe la dunia.

Hata hivyo Uingereza watakuwa na kazi ya ziada dhidi ya New Zealand ambao wamekuwa ni wababe wa mchezo huo kwa miaka ya hivi karibuni wakishinda kombe la dunia mara mbili mfululizo 2007, 2015.

Mara baada ya mchezo huo kocha wa Uingereza, Eddie Jones amesema kuwa licha ya kuwa wamekuwa wanapata matokeo ya ushindi na kusonga mbele lakini bado hajaridhishwa na kiwango cha timu yake.

"Nafurahi tumekuwa tunapata matokeo mazuri lakini sifurahishwi na kiwango cha uchezaji wa timu yangu, kama kweli tunataka kufanya vizuri zaidi ya hapa inabidi tubadilike sana kwenye upande wa kiuchezaji," amesema Jones.


Imeandaliwa na Badrudin Yahaya