US Open: Rafael Nadal Njia Nyeupe Grand Slam Ya 19

5th September 2019

CALIFORNIA, Marekani- Mcheza tenesi namba mbili kwa ubora duniani kwa upande wa wanaume, Rafael Nadal amefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya US Open baada ya kumchakaza Diego Schwartzman kwenye mchezo mkali wa robo fainali. Mhispania huyo anapewa nafasi kubwa ya kushinda taji hilo na kufikisha Grand Slam ya 19 ikiwa ni moja nyuma ya kinara Roger FedererĀ  ambaye tayari ameshatupwa nje ya michuano hii. Nadal, 33, alikutana na upinzani mkali kutoka kwa Muargentina, Schwartzman lakini mwisho wa mchezo alifanikiwa kuibuka na ushindi wa seti 6-4 7-5 6-2. Kwa matokeo hayo, Nadal sasa atacheza nusu fainali dhidi ya Muitalia, Marco Berrettini ambaye naye amefuzu kwenye hatua hiyo baada ya kumfunga Gael Monfils kwenye mchezo mwingine wa robo fainali. Nadal anapewa nafasi ya kunyakuwa taji hili baada ya kufuzu kwenye hatua ya nusu fainali na wapinzani watatu Berrettini, Diil Medvedev na Grigor Dimitrov ambao wote hawajawahi kucheza hatua ya fainali. Imeandaliwa na Badrudin Yahaya