UEFA: Samatta Awa Mtanzania Wa Kwanza Kufunga Bao Anfield, Genk Ikilala 2-1 Kwa Liverpool

6th November 2019

LIVERPOOL, Uingereza- Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta amefunga bao moja tamu sana kwenye uwanja wa Anfield lakini ameshindwa kuikoa timu yake ya KRC Genk na kipigo cha 2-1 kutoka kwa Livepool.

Mbwana Samatta
Mbwana Samatta
SUMMARY

Wenyeji Liverpool walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia kwa kiungo wao Georginio Wijnaldum lakini dakika tano kabla ya mapumziko Samatta aliisawazishia timu yake kwa bao safi la kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Bryan heynen.

Hilo ni bao la pili kwa Samatta kwenye michuano hiyo ya msimu huu huku akiwapiku mastaa wakubwa kama vile Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wenye bao moja kila mmoja hadi hivi sasa.

Kipigo walichokipata kutoka kwa Liverpool ni cha pili mfululizo ikiwa yamepita majuma mawili tangu walipofungwa 4-0 wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani nchini Ubelgiji.

Wenyeji Liverpool walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia kwa kiungo wao Georginio Wijnaldum lakini dakika tano kabla ya mapumziko Samatta aliisawazishia timu yake kwa bao safi la kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Bryan heynen.

Liverpool wakiwa nyumbani walicheza kwa kujiamini sana hasa kipindi cha pili na walifanikiwa kupata bao la ushindi lililofungwa na Alex Oxlade-Chamberlain akiitumia vyema pasi ya Mohamed Salah ndani ya boksi.

Matokeo hayo yanaipeleka Liverpool kileleni mwa msimamo wa kundi hilo baada ya kufikisha alama 9 huku Napoli wakishuka hadi nafasi ya pili wakiwa na alama 8 baada ya kubanwa kwa sare ya 1-1 dhidi ya RB Solzburg kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo.

RB Solzburg wao wana alama nne wakiwa kwenye nafasi ya tatu huku Genk wakiburuza mkia wakiwa na alama moja tu ikiwa imebakia michezo miwili kwa kila timu.

Timu mbili kutoka kila kundi zitafuzu kucheza hatua ya 16 wakati timu itakayomaliza nafasi ya tatu itafuzu kucheza kombe la Europa hatua ya 32 bora.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya