UEFA: PSG Wazidi Kumchongea Zidane Kwa Bosi Wake

19th September 2019

PARIS, Ufaransa -Angel Di Maria ameibuka shuja wa PSG baada ya kufanikiwa kufunga mabao mawili yaliyowezesha timu yake kuondoka na ushindi wa 3-0 mbele ya waajiri wake wa zamani Real Madrid.

Angel Di Maria
Angel Di Maria
SUMMARY

Baada ya Madrid kujaribu makocha wawili kuziba nafasi yake ilishindikana na kuamua kumrudia Zidane ambaye hakuwa na kipangamizi ambapo mwaka huu mwanzoni aliamua kurudi tena kwa mara ya pili.

Wakiwa wanapewa nafasi ndogo ya ushindi hasa baada ya kuwakosa nyota wake watatu upande wa ushambuliaji, Edson Cavan, Neymar na Kylian Mbappe, PSG walionekana kucheza kwa uelewano mzuri zaidi tofauti na ilivyokuwa kwa wapinzani wao ambao wamemuanzisha Eden Hazard kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe majira ya joto.

Matokeo hayo yanamuweka kocha Zinedine Zidane kwenye hali mbaye mbele ya mabosi wake ambao walikunjua hela ndefu kufanya maboresho ya kikosi chao kipindi cha usajili.

Zizou kama wengi wanavyopenda kumuita aliingia Real Madrid kwa mara ya kwanza akiwa kama kocha wa kikosi cha wakubwa mwaka 2016 ambapo alichukuwa nafasi ya Rafael Benitez na kwenda kuweka rekodi ya kuchukuwa taji la UEFA mara tatu mfululizo.

Hata hivyo mwaka 2018 aliamua kuachana na miamba hao kwa kile kinachoelezwa kuwa walishindwa kuelewana na uongozi wa juu unaoongozwa na Fiorentino Perez katika ishu za usajili.

Baada ya Madrid kujaribu makocha wawili kuziba nafasi yake ilishindikana na kuamua kumrudia Zidane ambaye hakuwa na kipangamizi ambapo mwaka huu mwanzoni aliamua kurudi tena kwa mara ya pili.

Takwimu Hazimbebi Kabisa

Tangu alipochukuwa timu kutoka kwa Sorano mwishoni mwa msimu uliopita Zidane ameshinda mechi chini ya asilimia 50 kitu ambacho kinaonesha si kizuri na huenda lolote linaweza kutokea hasa kwa Perez ambaye mara ya nyingi amekuwa si mtu mwenye uvumilivu kwa makocha.

Ukiachana na mechi hiyo, kipute kingine cha kufa mtu kilikuwa Vicente Calderon ambapo Atletico Madrid walikuwa wanawakaribisha Juventus na nyota wao Cristiano Ronaldo. 

Mabao ya Juan Cuadrado na Blaise Matuidi yalionekana kumaliza mchezo huo lakini Madrid waliamka mwishoni na kusawazisha kupitia kwa Stefan Savic na Hector Herrera na kuwafanya miamba hao kugawana alama.

Manchester City wakiwa na mpasuko kwenye safu yao ya ulinzi wameanza vyema michuano hii baada ya kuibuka na ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya Shakhtar Donetsk. Riyad Mahrez, Ilkay Gundogan na Gabriel Jesus ndo wafungaji wa mabao ya mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Uingereza.

Nao Tottenham Hotspurs wakiwa na uongozi wa 2-0 kupitia kwa Harry Kane na Lucs Moura wamejikuta wakilazimishwa sare na wenyeji wao Olympiakos ambao walisawzisha mabao yote mawili kupitia kwa Castelo Podence na Mathew Valbuena.

Matokeo Kamili

Club Brugge   0 0 Galatasaray

PSG 3-0 Real Madrid

Olympiakos 2-2 Spurs

Bayen Munich3-0 FK Crvena Zvezda

Dinamo Zegrab 4-0 Atalanta

Shakhatar 0-3 Man City

Atl Madrid 2-2 Juventus

B Leverkusen  1-2 Lokomotiv Moscow


Imeandaliwa na Badrudin Yahaya