UEFA: Magoli 8 Yafungwa Darajani, Chelsea Na Ajax Zikienda Sare, Dortmund Wakiinyuka Inter

6th November 2019

LONDON, Uingereza- Timu ya Chelsea ililazimika kupambana kuhakikisha walau wanapata alama moja mbele ya Ajax ambao hadi dakika ya 62 kipindi cha pili walikuwa mbele kwa mabao 4-1.

Chelsea vs Ajax
Chelsea vs Ajax
SUMMARY

Tukio hilo lilitokea kwenye dakika ya 68 ya mchezo ambapo Blind alimchezea faulo mbaya mshambuliaji, Tammy Abraham lakini Chelsea wakawa bado wanamliki mpira hivyo refa akawapa faida (advantage) ya kuendelea na shambulizi lao ambapo ilipofika ndani ya boksi ndipo Veltman akaunawa.

Mchezo huo uliokuwa mkali na wakusisimua ulishuhudiwa walinzi wa kati wa Ajax, Daley Blind na Joel Veltman wakilambwa kadi nyekundu kwa wakati mmoja huku wakiwa wamefanya makosa tofauti.

Tukio hilo lilitokea kwenye dakika ya 68 ya mchezo ambapo Blind alimchezea faulo mbaya mshambuliaji, Tammy Abraham lakini Chelsea wakawa bado wanamliki mpira hivyo refa akawapa faida (advantage) ya kuendelea na shambulizi lao ambapo ilipofika ndani ya boksi ndipo Veltman akaunawa.

Mwamuzi akatenga penati huku akiwapa kadi za njano Blind na Veltman na kwakuwa tayari walikuwa na kadi za njano ikabidi wote watoke nje kwa kadi nyekundu.

Kwenye mchezo huo Ajax ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Abraham ambaye alijifunga. Chelsea walichomoa kupitia kwa Gorginho aliyefunga kwa mkwaju wa penati.

Mlinda lango wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga alijifunga bao la pili baada ya kushindwa kuudhibiti mpira wa faulo uliopigwa na Hakim Ziyech. Donny van de Beek alifunga bao la tatu na Promes alifunga la nne.

Mabao ya Chelsea yamefungwa na Jorginho aliyefunga mara mbili kwa njia ya penati, Cezar Azpilicueta na Reece James.

Azpilicueta angefanikiwa kuwapa ushindi Chelsea kama si bao lake kukataliwa baada ya kuonekana kuwa aliunawa mpira kabla hajafunga bao la tano kwenye dakika za majeruhi.

Dortmund Wabadili Gia Angani

Huko Ujerumani, kwenye dimba la Signal Iduna Park, Borrusia Dortmund wakiwa nyumbani ilikuwa alimanusura wapigwe na Inter Milan kabla ya kuja kuibuka jioni na kushinda 3-2.

Wakiwa ugenini, Milan walipata mabao ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Lautaro Martinez na Matias Vecino na kuwafanya waongoze kwa 2-1 hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Dortmund walikuja kivingine na kufanikiwa kusawazisha mabao yote mawili kupitia kwa Achraf Hakim ambaye alifunga bao la kwanza na la tatu ambalo ni la ushindi. Bao la pili lilifungwa na Julian Brandt.

Barcelona Wakabwa Koo

Wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, Barcelona wameshindwa kutamba mbele ya Slavia Prague baada ya kulazimishwa sare ya 0-0.

Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa upande mmoja tumeshuhudia wenyeji Barcelona wakitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini washambuliaji wao wa mbele wakiongozwa na Lionel Messi walishindwa kutumbukiza mpira nyavuni.

Matokeo Kamili

Barcelona 0-0 Slavia Prague

Zenit 0-2 RB Leipzig

Liverpool 2-1 Genk

Napoli 1-1 RB Solzburg

Dortmund 3-2 Inter Milan

Lyon 3-1 Benfica

Chelsea 4-4 Ajax

Valencia 4-1 Lille

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya