Tetesi: Siku Za Kocha Mwinyi Zahera Zinahesabika Ndani Ya Yanga

5th November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Taarifa zilizoeneo kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini zinasema kuwa huenda uongozi wa Yanga umefikia maamuzi ya kumfuta kazi kocha wao Mwinyi Zahera.

Mwinyi Zahera
Mwinyi Zahera
SUMMARY

Walimu wanaotajwa kuchukuwa nafasi ya Zahera ni Hans van Pluijm na Kim Poulsen. Hata hivyo inasemekana kuwa endapo uamuzi huo utafikiwa kwa siku za hapa usoni, upo uwezekano wa kocha Charles Mkwasa kuchukuwa nafasi kwa muda.

Inasemekana kuwa maamuzi hayo yalishaamuliwa tangu awali lakini viongozi waliona ni vyema wasubiri kwanza timu itakapomaliza mchezo wa marudiano dhidi ya Pyramids ya Misri ambapo Yanga wamefungwa 3-0 siku ya Jumapili.

Kikosi cha Yanga kimetua nchini jana mchana wakitokea Misri na moja kwa moja timu imeingia kambini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ndanda utakaopigwa Mtwara kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Novemba 8.

Habari kutoka ndani ya klabu zinasema kuwa uongozi wa juu haufurahishwi na namna timu inavyocheza msimu huu pamoja na kauli za kocha ambazo mara kwa mara zimekuwa zikiwashutumu wachezaji pamoja na viongozi hadharani.

Walimu wanaotajwa kuchukuwa nafasi ya Zahera ni Hans van Pluijm na Kim Poulsen. Hata hivyo inasemekana kuwa endapo uamuzi huo utafikiwa kwa siku za hapa usoni, upo uwezekano wa kocha Charles Mkwasa kuchukuwa nafasi kwa muda.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya