Tetesi: Raheem Sterling Kufunika Mastaa Wote Kwa Mkwanja EPL

20th October 2019

MANCHESTER, Uingereza -Manchester City wanapanga kumuongezea mkataba mpya kiungo wa mshambuliaji Raheem Sterling ili kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi kwenye ligi ya Uingereza

Raheem Sterling
Raheem Sterling
SUMMARY

Manchester City wanapanga kumuongezea mkataba mpya kiungo wa mshambuliaji Raheem Sterling ili kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi kwenye ligi ya Uingereza na kuondoa uwezekano wa mchezaji huyo kujiunga na Real Madrid. (Sunday Express).


MANCHESTER, Uingereza -Manchester City wanapanga kumuongezea mkataba mpya kiungo wa mshambuliaji Raheem Sterling ili kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi kwenye ligi ya Uingereza na kuondoa uwezekano wa mchezaji huyo kujiunga na Real Madrid. (Sunday Express).

Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ametembelea mazoezini kwenye timu yake hiyo na kukutana na kocha Ole Gunnar Solskjaer siku ya Jumamosi wakati wa maandilizi kuelekea mchezo dhidi ya Liverpool utakaopigwa leo jioni. (Metro).

Klabu za Real Madrid na PSG zipo vitani kuwania saini ya kiungo raia wa Denmark na timu ya Tottenham Hotspurs, Christian Eriksen, 27. (Mail on Sunday).

Mwenyekiti wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis amekiri kuwa utafika wakati itabidi wamuuze mlinzi wao tegemezi Msenegal, Kalidou Koulibaly, 28 ambaye kwa muda mrefu amekuwa akiwandwa na Manchester United. (Sky Sport Italy).

Kiungo wa Real Madrid, Dani Ceballos, 23, amefanya mazungumzo na Florentino Perez na kumuomba amuuze moja kwa moja kwenye klabu ya Arsenal ambayo kwasasa anaichezea kwa mkopo. (Mail on Sunday).

Tottenham wanalenga kumsajili mlinzi wa pembeni wa West Brom, Nathan Ferguson, 19, ambaye pia klabu ya Crystal Palace imekuwa ikimfukuzia kwa karibu. (Sun on Sunday).

Kocha wa Aston Villa, Dean Smith amesema kuwa klabu yake haina mpango wa kumuuza kiungo wao fundi raia wa Scotland, John McGinn, 25 ambaye anatakwa na klabu kadhaa wakiwemo Manchester United. (Sunday Express).

Imeandaliwa na Jerry Mlosa