Tetesi: Paul Pogba Akutana Na Zinedine Zidane Uso Kwa Uso

18th October 2019

MANCHESTER, Uingereza- Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amekutana na kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane nchini Dubai kipindi cha mapumziko ya timu za taifa

Paul Pogba
Paul Pogba
SUMMARY

Taarifa za uvumi wa Paul Pogba kuhamia kwa matajiri hao wa jiji la Madrid zimezidi kushika kasi siku hadi siku hasa baada ya Mfaransa huyo kutoonesha kiwango kizuri katika timu yake ya Manchester United

MANCHESTER, Uingereza- Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amekutana na kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane nchini Dubai kipindi cha mapumziko ya timu za taifa kitendo ambacho kimeongeza uvumi kuwa huenda mchezaji huyo anaweza kuondoka Old Trafford kwenye kipindi kijacho cha usajili. ((Mirror).

Kiungo wa Barcelona, Ivan Rakitic, 31, ameondoa uwezekano wa kujiunga na Manchester United kipindi cha usajili wa Januari kwa kuwa familia yake haitaki kuhamia kwenye mji wa Manchester. (Mail).

Kocha wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino amesema hana mpango wa kuongeza mchezaji kwenye dirisha la usajili la Januari. (Mail).

Arsenal wanasadikika kuwa wameweka mezani kiasi cha paundi milioni 17.3 kwa ajili ya kunasa saidini ya kiungo mshambuliaji wa Real Madrid, Lucas Vazquez. (Sun)

Kocha wa zamani wa Juventus, Massimiliano Allegri amezidi kuongeza uvumi kwamba huenda akajiunga na Manchester United kwa siku za usoni baada ya kuweka wazi kuwa kwasasa anajifunza lugha ya kiingereza. (Mail)

Manchester City wameingia kwenye vita ya usajili na majirani zao Manchester United baada ya kujitosa kwenye dili la kumuwania mshambulia wa RB Solzburg, Erling Braut Haaland. ( Dail Mirror).

Chelsea chini ya kocha Frank Lampard wanamuwinda mchezaji kinda Emanuel Vignato, 19 lakini hawapo peke yao bali kuna timu nyingine nne zinamfuatilia kijana huyo. (Sun)

Inter Milan wanataka kumsajili kiungo wa Manchester United, Nemanja Matic, 31. (Sun).

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya