Tetesi: Mwinyi Zahera Kuamua Hatima Ya Niyonzima Ndani Ya Yanga

18th October 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania-Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema hawatakuwa na tatizo kumrejesha kiungo wao wa zamani Haruna Niyonzima kama kocha Mwinyi Zahera atamuhitaji.

Haruna Niyonzima
Haruna Niyonzima
SUMMARY

"Suala la kama tutamsajili au la litategemea na maoni ya kocha kwani yeye ndiye anayefahamu mapungufu ya timu yake," amesema Msolla.

Baada ya hivi karibuni Niyonzima kukutana na mmoja wa mabosi wanaohusika na masuala ya usajili Yanga, Abdallah Bin Kleb, kumekuwa na taarifa kuwa Niyonzima anaweza kurejeshwa wakati wa usajili wa dirisha.

Mwenyewe Niyonzima ameeleza kuwa yupo tayari kurejea Yanga, akikiri kuwa ni klabu aliyoitumikia kwa mapenzi makubwa.

Dk Msolla amesema pamoja na kuvutiwa na kiwango cha nyota huyo, hatma yake iko mikononi mwa Zahera.

"Ipo wazi Niyonzima aliitumikia Yanga kwa mapenzi yote na alifurahia uwepo wake katika klabu"

"Suala la kama tutamsajili au la litategemea na maoni ya kocha kwani yeye ndiye anayefahamu mapungufu ya timu yake," amesema Msolla.

Kwa mara ya kwanza, Niyonzima alitua Yanga mwaka 2012 akitokea APR na kufanikiwa kushinda mataji manne ya ligi kuu.

Mwaka 2017 alijiunga na Simba klabu aliyoitumikia kwa misimu miwili na kuongeza mataji mengine mawili ya ligi kuu.

Hata hivyo alishindwa kuelewana kuhusu mkataba mpya na tomu hiyo na ndipo alipoamua kurudi nchini Rwanda ambapo kwasasa anacheza kwenye klabu ya AS Kigali.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya