Tetesi: Lionel Messi Afichua Mipango Wa Neymar Kujiunga Na Barcelona

19th October 2019

BARCELONA, Hispania- Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, 32, amesema kuwa kuna baadhi ya watu ndani ya timu hawataki Neymar, 27, asajiliwe tena kwa mara ya pili kujiunga na timu hiyo. (Sun).

Neymar
Neymar
SUMMARY

Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, 32, amesema kuwa kuna baadhi ya watu ndani ya timu hawataki Neymar, 27, asajiliwe tena kwa mara ya pili kujiunga na timu hiyo. (Sun).

Manchester United wanalenga kufanya usajili wa kiungo wa zamani wa Liverpool anayecheza Juventus kwa sasa Emre Can, 25, kwenye dirisha la usajili Januari. Mchezaji huyo alijiunga na Juve mwaka 2018. (Sky Sport).

Liverpool na Chelsea zipo vitani kuwania saini ya kiungo wa Bournemouth raia wa Uingereza, Lewis Cook, 22. (Mail).

Kiungo wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Arsenal, Mesut Ozil, 31 anaamini kuwa amefanywa kuwa mbuzi wa kafara kila timu inapofanya vibaya hata hivyo amesema atabaki klabuni hapo hadi mkataba wake utakapofika tamati mwaka 2021. (Times)

Klabu ya Manchester City wamepanga kumpa mkataba mpya mshambuliaji wao Raheem Sterling ikiwa ni kpindi cha chini ya mwaka mmoja tangu aliposaini mkataba huu alionao kwa sasa. (Metro).

Mshambuliaji wa LA Galaxy ya Marekani, Zlatan Ibrahimovic huenda akastaafu soka siku ya Jumapili baada ya mechi yao ya mtoano. (Sun).

Mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo anavuna kiasi cha paudi milioni 37 kwa mwaka kupitia akaunti yake ya Instagram ikiwa ni fedha nyingi kuliko anazolipwa na klabu yake ya Juventus. (Sun).

Tottenham Hotspurs na Manchester United wanatarajia kuvutana kuwania saini ya kiungo wa Borussia Monchengladbach, Denis Zakari. (Dail Star).


Imeandaliwa na Badrudin Yahaya