Tetesi: Chelsea Watenga Paund Mil 150 Kuwashusha Zaha Na Timo Warner Januari

5th November 2019

LONDON, Uingereza -Winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha, 26, na mshambuliaji wa RB Leipzig, Timo Werner, 23, wapo kwenye orodha ya nyota ambao wanatakiwa kusajiliwa na Chelsea kwenye dirisha la mwezi Januari

Wilfred Zaha
Wilfred Zaha
SUMMARY

Inaaminika kwamba Chelsea wametenga kitita cha paundi milioni 150 kwa ajili ya kufanya usajili dirisha la mwezi Januari endapo adhabu yao ya kutokusajili itafunguliwa. (Telegraph).

LONDON, Uingereza -Winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha, 26, na mshambuliaji wa RB Leipzig, Timo Werner, 23, wapo kwenye orodha ya nyota ambao wanatakiwa kusajiliwa na Chelsea kwenye dirisha la mwezi Januari kama watafunguliwa kwenye adhabu yao ya kutokusajili. (Express).

Mil 150 Yatengwa Januari

Inaaminika kwamba Chelsea wametenga kitita cha paundi milioni 150 kwa ajili ya kufanya usajili dirisha la mwezi Januari endapo adhabu yao ya kutokusajili itafunguliwa. (Telegraph).

Bale Na Mil 70 Kumng'oa Sterling

Real Madrid wanajiaandaa kumtoa winga wa Wales, Gareth Bale, 30, pamoja na paundi milioni 70 kwa ajili ya kuinasa saini ya winga wa Manchester City Raheem Sterling, 24, (Sky Sports).

Man United v Liverpool Vitani

Manchester United na Liverpool kwa pamoja wanamfukuzia nyota wa Leipzig, Timo Werner lakini wababe hao wa Ujerumani wamewapa onyo timu hizo za England kwamba mshambuliaji huyo aendi popote. (Mirror).

Declan Rice atua kwenye rada za Solskjaer

Manchester United wanamuona kiungo wa West Ham na timu ya Taifa ya England, Declan Rice,20, kama chaguo lao namba moja kwa msimu ujao.(Goal).

Chelsea Wanataka Mshambuliaji mpya

Chelsea wameingia kwenye mbio ya kumnasa mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembele, 23, na nyota huyo wa zamani wa Celtic pia amekuwa akihusishwa na kujiunga na Manchester United. (Mail).

Mourinho apigiwa debe Bayern

Kwa mujibu wa nyota wa zamani wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger amesema kwamba itakuwa vizuri kama Kocha wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho atainoa Bayern Munich(Evening Standard).

Kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger ni miongoni mwa makocha ambao wanapewa nafasi ya kurithi mikoba ya Niko Kovac . (Guardian).

Pogba kuendelea kukaa nje

Manchester United wataendelea kuikosa huduma ya kiungo wake wa Ufaransa Paul Pogba, 26, kwa zaidi ya wiki nne kutokana na kusumbuliwa na tatizo la enka. (ESPN).

Wolves waenda Italia kusaka kiungo

Wolves wanajiaandaa kutuma paundi milioni 13 kwa ajili ya kiungo wa Kiswedish na klabu ya Atalanta Dejan Kulusevski, 23, ambaye pia alikuwa akihusishwa na klabu za Manchester City na Arsenal.(Sport Witness).

Man United  wamkazia Smalling

Manchester United wamekataa ofa ya paundi milioni 13 kwa mlinzi wake Chris Smalling, 29, ambaye yupo kwa mkopo AS Roma. (Star)

Timu za EPL vitani kwa Msenegali

Newcastle na Leicester City wanamfukuzia mshambuliaji wa Senegal na klabu ya Metz Habib Diallo,24,. (Express)

Imeandaliwa na Jerry Mlosa