Tennis: Serena Williams Atinga Fainali Ya US Open

6th September 2019

NEW YORK, Marekani- Mwana dada Serena Williams amefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya US Open baada ya kumfunga Elina Svitolina kwenye mchezo wa nusu fainali. Williams, 37, ameshinda kwa jumla ya seti 6-3 6-1 dhidi ya Svitolina ambaye ni namba tano kwa ubora. Kwa matokeo hayo Williams atakumbana na Mcanada, Bianca Andreescu kwenye fainali inayotarajiwa kuchezwa Jumamosi. Mpinzani wake Andreescu amefanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo baada ya kumfunga Mswizi, Belinda Bencic kwa jumla ya seti 7-6 7-3 7-5. Andreescu ambaye anacheza kwa mara ya kwanza michuano ya US Open alizaliwa miezi tisa baada ya Williams kushinda Grand Slam yake ya kwanza mwaka 1999. Imeandaliwa na Badrudin Yahaya