Tennis: Rafael Nadal Atwaa Grand Slam Ya 19 Baada Ya Kumtwanga Mrusi Fainali Ya US Open

9th September 2019

Rafael Nadal Atwaa Grand Slam Ya 19 Baada Ya Kumtwanga Mrusi Fainali Ya US Open

SUMMARY
  • Rafael Nadal Atwaa Grand Slam Ya 19 Baada Ya Kumtwanga Mrusi Fainali Ya US Open
NEW YORK, Marekani -Mcheza Tennis namba mbili kwa ubora kwa upande wa wanaume, Rafael Nadal amethibitisha ubora wake baada ya kuibuka kidedea kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Mrusi, Daniil Medvedev na kufanikiwa kushinda taji la US Open huku ikiwa ni Grand Slam yake ya 19. Katika mchezo huo wa fainali ambao ulikuwa ni mkali na wakusisimua, Nadal ameshinda kwa jumla ya seti 7-5 6-3 5-7 4-6 6-4. Nadal, 33, aliongoza vizuri kwenye seti mbili za mwanzo kabla ya Medvedev kuamka na kusawazisha kitu ambacho kilisababisha mchezo huo kuingia kwenye seti ya ziadi ya kuamua mshindi (decider). Hata hivyo Nadal alipambana na kushinda vikwazo vyote na kushinda taji hilo kwenye fainali ambayo imechezwa kwa saa nne na dakika 50 ikiwa ni dakika nne pungufu ya fainali ambayo imeweka rekodi ya kuchezwa kwa muda mrefu zaidi. Ushindi wa Nadal unamfanya kufikisha Grand Slam 19 ikiwa ni moja nyuma ya Mswiz, Roger Federer ambaye anashikilia rekodi ya kuwa na Grand Slam 20 kwa upande wa wanaume. "Huu ni mmoja kati ya usiku bora kwenye maisha yangu ya Tennis, ilikuwa ni mechi ngumu na fainali bora kabisa," amesema Nadal baada ya kutangazwa bingwa. Imeandaliwa na Badrudin Yahaya