Tennis: Rafael Nadal Aipaisha Hispania Kushinda Davis Cup

25th November 2019

MADRID, Hispania- Wenyeji wa michuano ya Davis Cup, timu ya taifa ya Hispania wamefanikiwa kushinda taji hilo kwa kuwafunga Canada kwenye mchezo mkali wa fainali uliofanyika usiku wa kuamkia leo.

Rafael Nadal
Rafael Nadal
SUMMARY

Zamu ya Nadal kuingia uwanja ilifika na kukutana na Shapovalov ambapo mchezo huo ulitarajiwa kuwa na mshike mshike wa aina yake lakini nyota huyo ambaye wiki iliyopita alishindwa kubeba taji la ATP, safari hii alishinda na kuwafanya wenyeji kuwa mbele kwa 2-0.

Nyota anayeshikilia nafasi ya kwanza kwa ubora duniani upande wa wanaume, Rafael Nadal ndiye aliyefanikisha ushindi huo baada ya kuibuka na ushindi wa seti 6-3 7-6 (9-7) dhidi ya Denis Shapovalov.

Fainali hiyo ilianza kwa mchezo kati ya Mhispania, Roberto Bautista Agut ambaye alimfunga Felix Auger-Aliassime kwa jumla ya seti 7-6 (7-3) 6-3 na kuwafanya wenyeji kuwa mbele kwa 1-0. 

Agut amecheza na kushinda mechi hiyo ikiwa ni siku tatu tu kupita tangu alipompoteza baba yake mzazi na baada ya ushindi huo alianguka chini huku akilia kwa kilio kikubwa.

Zamu ya Nadal kuingia uwanja ilifika na kukutana na Shapovalov ambapo mchezo huo ulitarajiwa kuwa na mshike mshike wa aina yake lakini nyota huyo ambaye wiki iliyopita alishindwa kubeba taji la ATP, safari hii alishinda na kuwafanya wenyeji kuwa mbele kwa 2-0.

Ushindi huo umewafanya Hispania kushinda taji lao la kwanza la tenesi tangu mara ya mwisho walipofanya hivyo mwaka 2011.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya