Tennis: Naomi Osaka Atupwa Nje US Open Huku Rafael Nadal Akitamba

3rd September 2019

NEW YORK, Marekani -Bingwa mtetezi wa michuano ya US Open kwa upande wa kina dada, Naomi Osaka ameondoshwa mashindanoni na Mswiz, Belinda Bencic ambaye amefuzu kucheza hatua ya robo fainali. Osaka, 21, alizidiwa kwenye hatua za mwisho wakati wa seti ya kwanza na baadaye kupotezwa kabisa katika seti ya tano ndani ya dimba la Arthur Ashe. Kwa matokeo hayo, Mjapani, Osaka atapoteza hadhi yake ya kuwa mchezaji namba moja kwa ubora kwa upande wa wanawawake na nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na Muaustralia, Ashleigh Barty ambaye amekuja juu kwa siku za hizi karibuni. Bencic ambaye anatajwa kuwa mchezaji nambna 13 kwa ubora atakutana na Donna Vekik kwenye hatua ya robo fainali. Djokovic nje Kwenye michezo ya jana pia tulishuhudia bingwa mtetezi wa michuano hiyo kwa upande wa wanaume Novak Djokovic akiondoshwa na Stan Wawrinka. Katika michezo mingine iliyopigwa leo kwa upande wa wanaume, Rafael Nadal amefanikiwa kusonga mbele baada ya ushindi wa 6-3 3-6 6-1 6-2 dhidi ya Marin Cilic. Kwa matokeo hayo, Nadal raia wa Hispania mwenye grand slam 18 amefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano hiyo na atavaana na Muargentina Diego Schartzman. Imeandaliwa na Badrudin Yahaya