Tennis: Naomi Osaka Amkalisha Ashleigh Barty Na Kushinda China Open

7th October 2019

BEIJING, China- Naomi Osaka amefanikiwa kushinda taji la China Open baada ya kumfunga mchezaji namba moja kwa ubora kwa upande wa kina dada Ashleigh Barty.

Naomi Osaka
Naomi Osaka
SUMMARY

Kabla ya mchezo huo wa fainali miamba hao walikuwa wamekutana mara tatu ambapo Barty alikuwa anaongoza kwa kuibuka na ushindi mara mbili dhidi ya moja ya Osaka.

Osaka ameshinda kwa jumla ya seti 3-6 6-3 6-2 na kufanikiwa kushinda taji lake la pili mfululizo baada ya Pan Pacific Open aliloshinda mwezi uliopita.

Mwana dada huyo kwasasa yupo moto kweli kweli hiyo ikiwa ni mechi yake ya 10 mfululizo anaibuka na ushindi tangu mara ya mwisho alivyofungwa kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya US Open.

Ushindi huo unamfanya Osaka kuwa na rekodi sawa ya kufungana dhidi ya Barty.

Kabla ya mchezo huo wa fainali miamba hao walikuwa wamekutana mara tatu ambapo Barty alikuwa anaongoza kwa kuibuka na ushindi mara mbili dhidi ya moja ya Osaka.

Mapema mwaka huu Barty ndiye aliyemuengua Osaka kileleni akimpiku katika nafasi ya kwanza kwa ubora.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya