Tennis: Coco Gauff Aweka Rekodi Ya Dunia, Medvedev Ashinda Shanghai Masters

14th October 2019

SHANGHAI, China- Mwana dada mchezaji wa tennis Coco Gauff ameweka rekodi ya kushinda taji akiwa na umri mdogo zaidi kwenye historia ya mchezo huo baada ya kufanikiwa kunyakuwa Linz Open.

Medvedev
Medvedev
SUMMARY

Medvedev ndiye mchezaji aliyecheza fainali nyingi msimu huu kuliko mchezaji mwingine yeyote na huu ni ubingwa wake wa nne mwaka huu.

Guaff, 15, ameshinda taji hilo akimfunga Jelena Ostapenko kwa jumla ya seti 6-3 1-6 6-2 na anatarajiwa kuingia kwenye 75 bora ya wachezaji wa dunia.

Mchezaji huyo alifuzu kwa bahati kushiriki kwenye michuano hiyo baada ya kupoteza kwenye mchezo wa mwisho wa mchujo.

Jina la kinda huyo raia wa Marekani lilianza kuchomoza mapema mwaka huu baada ya kufanikiwa kumdfunga Venus Williams kwenye mzunguko wa kwanza wa michuano ya Wimbledon.

Kwasasa Gauff anakuwa ameyafikia mafanikio ya mwana dada mwenzie Nicole Vadisova ambaye naye alishinda taji la Tashkent Open mwaka 2004 akiwa na umri huo wa miaka 15.

"Imekuwa ni wiki bora sana kwangu, nimatumaini yangu nitarejea tena hapa kwa wakati mwingine, tukio hili sitalisahau kwenye maisha yangu yote," amesema Gauff.

Kwa upande wa wanaueme, mchezaji tenesi raia wa Urusi, Daniil Medvedev ameshinda taji la Shanghai Masters baada ya kumfunga Alexander Zverev kwenye mchezo wa fainali uliofanyika siku ya Jumapili.

Mchezaji huyo namba nne kwa ubora ameshinda kwa seti 6-4 6-1 kwenye mchezo uliodumu kwa muda wa dakika 73.

Medvedev ndiye mchezaji aliyecheza fainali nyingi msimu huu kuliko mchezaji mwingine yeyote na huu ni ubingwa wake wa nne mwaka huu.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya