Tennis: Andy Murry Atakata, Kyle Edmund Atupwa Nje Shanghai Open

8th October 2019

SHANGHAI, China- Bingwa zamani wa mchezo wa tenesi Andy Murry ameanza vizuri michuano ya Shanghai Open baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Juan Londero.

Andy Murray
Andy Murray
SUMMARY

Murry ana historia nzuri na michuano ya Shanghai Open akiwa tayari ameshashinda taji mara tatu miaka ya 2010, 2011 na 2016.

Murray ameshinda kwa jumla ya seti 2-6 6-2 6-3 kwenye mchezo ambao alianza kwa kufunngwa vibaya kwenye seti ya kwanza kitu kilichoanza kutia mashaka miongoni mwa mashabiki wake.

Mapema mwezi huu mcheza tenesi huyo raia wa Uingereza alifanikiwa kucheza robo fainali ya michuano ya China Open ikiwa ni mara yake ya kwanza kwa kipindi cha mwaka mzima.

Murry ana historia nzuri na michuano ya Shanghai Open akiwa tayari ameshashinda taji mara tatu miaka ya 2010, 2011 na 2016.

Kwenye mchezo mwingine, mchezaji namba moja kwa ubora nchini Uingereza, Kyle Edmund amepoteza mchezo wake wa kwanza tu dhidi ya Jeremy Chardy raia wa Ufaransa.

Edmund amefungwa kwa jumla ya seti 6-4 7-6 (7-3) na sasa yupo kwenye hati hati ya kupoteza hadhi yake ya ubora kwa mujibu wa viwango vinavyotarajiwa kutolewa wiki ijayo.

Hiki ni kipigo cha sita kwa nyota huyo ambaye mara ya mwisho kuibuka na ushindi ilikuwa ni mwezi Agosti pale alipocheza dhidi ya Nick Kyrgios kwenye michuano ya Rogers Cup.

Dan Evans au Cameron Norrie wanatazamiwa kumshusha Edmund kwenye nafasi yake ya kwanza kwa ubora nchini Uingereza.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya