Tenesi: Stefanos Tsitsipas Ambwaga Dominic Thiem Na Kutwaa Ubingwa Wa ATP

18th November 2019

LONDON, Uingereza- Stefanos Tsitsipas ametoka seti moja nyuma na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 6-7 (6-8) 6-2 7-6 (7-4) dhidi ya Dominic Thiem na hivyo kufanikiwa kushinda taji la michuano ya ATP (nane bora).

Stefanos Tsitsipas
Stefanos Tsitsipas
SUMMARY

Ushindi huu kwa Tsitsipas unamfanya kuingia kwenye rekodi ya kuwa bingwa wa michuano hii mwenye umri mdogo tangu mwaka 2001 ambapo Muaustralia Lleyton Hewitt naye alipofanya hivyo.

Hili ni taji la kwanza kubwa kwa Tsitsipas mwenye umri wa miaka 21 raia wa Ugiriki ambaye dhahiri alionekana kupotezwa kwenye seti ya kwanza.

Thiem 26, itabidi ajilaumu mwenyewe kwani kasi aliyoanza nayo kwenye seti ya kwanza ilijikuta ikipotea kadiri muda ulivyokuwa unakwenda na alijikuta akianza kufanya makosa mengi ambayo yamemgharimu.

Ushindi huu kwa Tsitsipas unamfanya kuingia kwenye rekodi ya kuwa bingwa wa michuano hii mwenye umri mdogo tangu mwaka 2001 ambapo Muaustralia Lleyton Hewitt naye alipofanya hivyo.

"Hizi ni ndoto ambazo zimekuwa kweli, nilikuwa nahisi wasiwasi katika baadhi ya matukio lakini nilijitahidi kukiweka kichwa changu sawa na hiyo ndiyo ilikuwa siri ya ushindi huu," amesema Tsitsipas.

Kwenye michuano hii ambaye ilianza tangu wiki iliyopita ilishirika wachezaji nane ambao wana nafasi za juu kwa ubora.

Wachezaji walioshiriki ni Tsitsipas, Thiem, Rodger Federer, Rafael Nadal, Novak Djokovic, Matteo Berrettin, Alexander Zverev na Daniil Medvedev.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya