Tenesi: Novak Djokovic Ashinda Taji La Tano La Paris Masters

4th November 2019

PARIS, Ufaransa- Mchezaji tenesi namba moja duniani kwa upande wa wanaume, Novak Djokovic ameshinda taji la Paris Masters baada ya kumfunga Denis Shapovalov kwenye mchezo wa fainali.

Novak Djokovic
Novak Djokovic
SUMMARY

Licha ya ushindi huo lakini bado Djokovic anatarajia kupoteza hadhi yake ya namba moja kwa ubora duniani mbele ya Mhispania, Rafael Nadal wakati viwango vipya vitakapotangazwa siku ya leo.

Djokovic ameshinda kwa seti 6-3 6-4 na kufanikiwa kushinda taji la tano kwenye michuano hiyo.

Huu pia ni ushindi wa nne kwa Djokovic dhidi ya Shapovalov ambaye anashika nafasi ya 28 kwa ubora duniani.

Kwenye michuano hii msimu uliopita, Djokovic alipoteza kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Karen Khachanov. Hata hivyo hakukuwa na makosa tena safari hii kwa Mserbia huyo mwenye umri wa miaka 32.

Licha ya ushindi huo lakini bado Djokovic anatarajia kupoteza hadhi yake ya namba moja kwa ubora duniani mbele ya Mhispania, Rafael Nadal wakati viwango vipya vitakapotangazwa siku ya leo.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya