Sudan v Taifa Stars: Erasto Nyoni Asema Leo Ni Kufa Au Kupona

18th October 2019

KHARTOUM, Sudan- Mlinzi wa kati wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Simba, Erasto Nyoni amesema kuwa mchezo wa leo dhidi ya Sudan ni wa kufa au kupona.

Taifa Stars
Taifa Stars
SUMMARY

Stars chini ya kaimu kocha mkuu Etiene Ndayiragije wamecheza jumla ya dakika 540 (mechi 6) bila kuondoka na ushindi ndani ya dakika 90 huku pia wakiwa wamefunga mabao mawili tu yalioyofungwa na wachezaji ambao hawapo kwenye mchezo wa leo dhidi ya Sudan (Msuva, Samatta).

Stars wanashuka dimbani leo majira ya saa mbili usiku kupambana na Suda kwenye mchezo wa kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya CHAN itakayofanyika nchini Cameroon.

Huu ni mchezo wa pili kwa miamba hao kwani kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es saalam, Tanzania, Septemba 20, mwaka huu Stars walifungwa kwa bao 1-0.

Ili Stars waweze kukata tiketi kwenye mchezo wa leo wanahitajika kushinda kwa mabao mawili na zaidi.

Akizungumza moja kwa moja kutokea Sudan, Nyoni ambaye pia ni nahodha msaidizi wa kikosi hicho amesema kuwa wachezaji wote wanajua umuhimu wa mchezo wa leo na kwamba yeyote atakaye pata nafasi ya kucheza basi anajua nini cha kufanya.

"Tangu tulivyopoteza mchezo wa kwanza tumeelewa nini lilikuwa kosa letu na kupitia program mbalimbali tulizopewa na walimu wetu tunaimani kuwa mchezo wa leo utakuwa ni mgumu kwa pande zote mbili lakini kwetu huu ni mchezo wa kufa au kupona," amesema Nyoni.

Kabla ya kwenda Sudan , Stars walikwa nchini Rwanda ambapo Oktoba 14, walicheza mchezo wa kujipima ubavu na matokeo yalikuwa ni 0-0.

Stars chini ya kaimu kocha mkuu Etiene Ndayiragije wamecheza jumla ya dakika 540 (mechi 6) bila kuondoka na ushindi ndani ya dakika 90 huku pia wakiwa wamefunga mabao mawili tu yalioyofungwa na wachezaji ambao hawapo kwenye mchezo wa leo dhidi ya Sudan (Msuva, Samatta).

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya