SportPesa Jackpot: Hata Wanawake Nao Wamo Kwenye Msako Wa Mamilioni (Sehemu Ya Mwisho)
30th October 2019
DAR ES SALAAM, Tanzania -Katika toleo lililopita tulimzungumza na Bi Scolastica Ngwalueson ambaye aliibuka mshindi wa SportPesa Jackpot akijinyakulia donge nono la Tsh 260,319,980.

Hata wewe unaweza kushinda
Hata wewe unaweza kuibuka Milionea kama ilivyokuwa kwa Scolastika. Kitita cha Tsh 272,715,860 za SportPesa Jackpot kipo mezani wikiendi hii.
Bofya HAPA kubashiri mechi 13 kwa usahihi uwe Milionea na ukipatia mechi 10, 11 au 12 kuna BONUS za kibabe.
Katika makala hiyo tuliongea na mume wa mshindi Bwana Ally Katundu pamoja na kaka yake, Edgar Ngwalueson ambao kwa pamoja walisema kuwa hawaoni ajabu kwa mwanamke kujihusisha na michezo ya kubashiri kama wanaume wanavyofanya
Bi Scolastika elienda mbali zaidi na kuweka wazi kuwa hana mpango tena wa kuendelea na maisha yake ya kujitafutia riziki kwa kupitia biashara yake ya mihogo na kwamba hivi sasa ataanza kupanga mipango mipya ya kimilionea.
Soma sehemu ya kwanza -SportPesa Jackpot: Hata Wanawake Nao Wamo Kwenye Msako Wa Mamilioni (Sehemu Ya 1)
Katika muendelezo wa mahojiano yake na SportPesa News, Bi Scolastika pamoja na familia yake wameweka hadharani baadhi ya mipango yao mara baada ya kushinda kitita hicho cha fedha.
Elimu bora
Edgar ambaye ni kaka wa Scola amemkumbusha dada yake kuhusu familia yao na kwamba fedha hizo zitumike vizuri kwa ajili ya kuwainua wote kwa pamoja.
"Mimi nina watoto wangu lakini hata yeye Scola ana watoto wake pia tunaye mdogo wetu wa mwisho, wote hao wanahitaji elimu bora hivyo nadhani huu ni muda sahihi wa kufanya hivyo kutokana na hela tuliyoshinda," amesema Edgar ambaye mara kadhaa ndiyo amekuwa akimjengea beti dada yake.
Bi Scola anaanza kwa kuwa ushauri wanawake wote nchini ambao wamekuwa na tabia ya kupuuza na kubeza michezo ya beti na wengine wakiamini kuwa wanaopaswa kucheza ni wanaume tu.
Scola Katusua; Bi Scolastica Akabidhiwa Hundi Baada Ya Kushinda SportPesa Jackpot Ya Tsh 260,319,980
Nyumba kwanza
Mbali na Edgar kukazia katika suala zima la watoto wao na mdogo wao wa mwisho, Lakini Bi Scola kwa upande wake anawaza kushusha mjengo wa maana kabla ya kuanza kutafakari vitu vingine vya ziada.
"Najua kuna mambo mengi ya kufanya lakini cha kwanza ambacho kwangu naona ni muhimu ni kujenga eneo langu zuri la kuishi (nyumba) halafu baada ya hapo ndio nitajua vitu gani vingine vifuate," amesema Scola.
Wanawake Tuchangamkieni Fursa
Scola amemalizia kwa kutoa rai kwa wanawake wenzake akiwaaambiwa washiriki kwenye mchezo ya kubashiri na kampuni ya SportPesa kwani na wao wanaweza wakapata nafasi ya kubadilisha maisha yao kama ilivyotokea kwa upande wake.
"Mchezo wa kubashiri siyo kwa ajili ya wanaume tu."
"Mi nawashauri wanawake wenzangu msipuuze huu mchezo mkaona kama nyie hauwahusu, hata nyinyi mnaweza mkacheza na mkashinda kama ilivyotokea kwangu, hivyo ni kazi kwenu tu kutafuta msaada kwa watu wenu wa karibu ili kujua namna ya kucheza,"alihitimisha.
Hata wewe unaweza kushinda
Hata wewe unaweza kuibuka Milionea kama ilivyokuwa kwa Scolastika. Kitita cha Tsh 272,715,860 za SportPesa Jackpot kipo mezani wikiendi hii.
Bofya HAPA kubashiri mechi 13 kwa usahihi uwe Milionea na ukipatia mechi 10, 11 au 12 kuna BONUS za kibabe.
Imeandaliwa na Badrudin Yahaya na kuhaririwa na Adam Mbwana