Shanghai Masters: Federer, Djokovic Wakumbana Na Vipigo Robo Fainali

12th October 2019

SHANGHAI, China- Novak Djokovik na Roger Federer wameshindwa kutoboa kwenye michezo yao ya robo fainali ya michuano ya Shanghai Masters baada ya kukumbana na vipigo vilivyowafanya kutupwa nje ya mashindano hayo.

Novak Djokovic
Novak Djokovic
SUMMARY

Kwa matokeo haya sasa Tsitsipas atacheza dhidi ya Daniil Medvedev ambaye amemfunga Fabio Fognini kwenye hatua ya nusu fainali wakati nusu fainali ya pili itakuwa ni kati ya Zverev dhidi ya Matteo Berrettin.

Djokovik ambaye ni mchezaji namba moja kwa ubora na bingwa mtetezi wa michuano hiyo amefungwa na Stefanos Tshtsipas kwa jumla ya seti 3-6 7-5 6-3.

Naye Federer amefungwa na Alexender Zverev kwa jumla ya seti 6-3 6-7 (7-9) 6-3.

Kwa matokeo haya sasa Tsitsipas atacheza dhidi ya Daniil Medvedev ambaye amemfunga Fabio Fognini kwenye hatua ya nusu fainali wakati nusu fainali ya pili itakuwa ni kati ya Zverev dhidi ya Matteo Berrettin.

Berrettin kwa upande wake yeye amemfunga Dominic Thiem kwenye mchezo wa robo fainali ambao umefanyika jana.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya