Pre- Season: Matokeo Ya Mechi Zote Za Kirafiki Kwa Timu Zinazoshiriki NBA

16th October 2019

SHANGHAI, China- Ikiwa zimebaki siku takribani tano kabla ya ligi kuu ya kikapu ya nchini Marekani maarufu NBA, kuanza, maandalizi yameendelea kushika kasi kwenye mechi za kujiweka sawa huko nchini China.

NBA
NBA
SUMMARY

Carsen Edwards amefunga pointi tatu mara nane na kufanikiwa kufunga vikapu 26 kwa upande wa Celtic vilivyoiwezesha timu yake kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Cavaliers na kuwafanya kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa kwenye pre season hadi hivi sasa.

Kikawaida timu zinazoshiriki ligi hiyo huwa zinaweka kambi China kwa ajili ya kucheza michezo ya kirafiki na kujiweka sawa.

Mamlaka za usimamizi wa NBA zilianzisha utaratibu huo tangu mwaka 2011 ikiwa ni sehemu ya matangazo na kuongeza kipato kwenye mchezo huo unaosadikika kuwa na utajiri mkubwa duniani.

Yafauatyo ni matokeo ya mechi mbalimbali za kirafiki zilizochezwa usiku wa kumkia leo kama yanavyoletwa kwenu na mwandishi wa SportPesa News.

Detroit Pistons 86-106 Philadephia 76ers

Joel Embiid amefunga vikapu 24 kwenye mchezo huo na kuibuka nyota wakati akiisaidia timu yake ya Philadephia ikiibuka na ushindi mnono dhidi ya Pistons.

Licha ya kupoteza mchezo lakini Cristian Wood wa Pistons naye alionesha uwezo wake binafsi baada ya kufunga vikapu 19 huku mwenzie aitwaye Tony Snell akifunga vikapu 17.

Boston Celtics 118-95 Cleveland Cavaliers

Carsen Edwards amefunga pointi tatu mara nane na kufanikiwa kufunga vikapu 26 kwa upande wa Celtic vilivyoiwezesha timu yake kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Cavaliers na kuwafanya kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa kwenye pre season hadi hivi sasa.

Kwenye mauaji hayo, Tremont Waters pia amehusika kwani naye amefunga pointi tatu mara nane na kumfanya kuibuka na vikapu 24 kwenye mchezo huo.

Kwa upande wa Cavaliers, Collin Sexton ndiye alikuwa nyota baada ya kufanikiwa kufunga vikapu 20 huku Darius Garland naye kwa upande wake amefunga vikapu 16.

Minnesota Timberwolves 119-111 Indian Pacers

Karl-Anthony Towns amefunga vikapu 33 na kutengeneza assisti 4 akiisadia timu yake ya Minnesota kuwafunga Indian Pacer kwenye mchezo ulio kuwa ni wa vuta nikuvute.

Ribert Covington aliongeza vikapu 10 kwenye mchezo huo ambao kila mchezaji wa Minnesota aliyeanza alifunga vikapu 9.

Domantas Sabonis amefunga vikapu 11 kwa upande wa Indian Pacers na kwenye mchezo huo hakuna mchezaji mwingine wa Pacers aliyefikisha vikapu 10.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya