Pre-Season: LeBron James, Anthony Davis Wang'aa Lakers Wakiwatambia Warriors

6th October 2019

SAN FRANSCISCO, Marekani- Timu ya mpira wa kikapu ya Golden State Warriors imefungua uwanja wao kwa majanga baada ya kukubali kichapo cha vikapu 123-101 kutoka kwa Los Angeles Lakers.

Lakers
Lakers
SUMMARY

Kwa upande wao Warrior, nyota wao Stephen Curry kama kawaida alikuwa bora baada ya kufunga vikapu 18 ndani ya dakika 17 wakati Jordan Poole akifunga vikapu 17 ikiwa ni mchezo wake wa kwanza ndani ya timu hiyo.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza wa kutest mitambo kwa timu zote mbili kabla ya ligi ya NBA kuanza mnamo Oktoba 22, 2019.

Kwenye mchezo huo nyota wawili wa Lakers LeBron James na Anthony David ndiyo waliyojipakulia minyama zaidi baada ya kuonesha kiwango cha kukata na shoka.

Davis alikuwa bora sana kwenye mchezo huo baada ya kufunga vikapu 22 ndani ya dakika zake 18 za kwanza kwenye uzi wa Lakers ambayo amejiunga nayo msimu huu.

Naye LeBron hakuwa mbali kuonesha kiwango chake kwani alifunga vikapu 15 na kutengeneza assist nane ndani ya dakika 17 tu za mchezo.

Kwa upande wao Warrior, nyota wao Stephen Curry kama kawaida alikuwa bora baada ya kufunga vikapu 18 ndani ya dakika 17 wakati Jordan Poole akifunga vikapu 17 ikiwa ni mchezo wake wa kwanza ndani ya timu hiyo.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya