Pre-Season: LeBron James Afanya Maajabu Lakers Wakiikalisha Warriors

17th October 2019

SHANGHAI, China- Nyota wa Los Angeles Lakers, LeBron James ameongoza mauaji kwa timu yake wakifanikiwa kuwafunga Golden State Warriors kwa jumla ya vikapu 126-93 kwenye mchezo wa kirafiki.

Lebron James
Lebron James
SUMMARY

LeBron amefunga vikapu 18 na assisti 11 huku nyota mwingine wa timu hiyo Anthony Davis akifunga vikapu 8 na assist 8. Avery Bradley pia amefunga 18, Quinn Cook amefunga 16 kwa upande wa Lakers ambao kwa ujumla walifunga vikapu 104 ndani ya robo tatu tu.

LeBron amefunga vikapu 18 na assisti 11 huku nyota mwingine wa timu hiyo Anthony Davis akifunga vikapu 8 na assist 8. Avery Bradley pia amefunga 18, Quinn Cook amefunga 16 kwa upande wa Lakers ambao kwa ujumla walifunga vikapu 104 ndani ya robo tatu tu.

Kwa upande wa Warriors, D'Angelo Russell ndiye aliyeongoza mapambano kwa kufunga vikapu 23.

San Antonio Spurs 128-114 Houston Rockets

LaMarcus Aldridge amefunga vikapu 22 na kuwasaidia San Antonio kushinda mchezo huo dhidi ya Nicks huku huo ukiwa ndiyo ushindi wao wa kwanza wa mechi za kirafiki. Dejounte Murray naye amefunga vikapu 20 kwa upande wa San Antonio.

James Harden alijitahidi kuwabeba Rockets kwa kiasi kikubwa baada ya kufunga vikapu 40 peke yake lakini bado havijasaidia wao kupata ushindi.

Detroit Pistons 116-110 Charlotte Hornets

Andre Drummond na Markieff Morris wote wamefunga vikapu 17 huku Langston Galloway akiwa ndiye aliyefunga vikapu 18 vikiwa ni vingi kwa upande wa timu ya Pistons.

Malik Monk ameongoza kwa upande wa Charlotte akiwa amefunga vikapu 18 na assisti saba huku Cody Zeller alikuwa mmoja kati ya wachezaji wanne wa timu hiyo waliofunga vikapu 12.

Melbourne United 110-124 Sacramento Kings

Marvin Baley III amefunga vkapu 30 huku Yogi Ferrell akifunga 24, naye Harrison Barnes akifunga 18 kwa upande wa Kings ambao ndiyo wameibuka washindi wa mchezo huo.

Cris Gouiding amefunga vikapu 25 kwa Melbourne, naye Melo Trimble ameongeza 20 huku Shawn Long akifunga 15 kwa upande wa timu yao licha ya kuwa wamefungwa.

Memphis Grizzlies 124-119 Oklahoma City Thunder

Oklahoma City Thunder wamepoteza mchezo huo kutokana na kiwango bora cha mchezaji wa Memphis, Dillon Brooks ambaye peke yake amefunga vikapu 30 kwenye mchezo huo. Mbali na Brooks lakini pia Tyus Jones amefunga vikapu 10.

Shai Gilgeous-Alexander amefunga vikapu 17 kwa upande wa Thunder huku Danilo Galinari akifunga vikapu 16 lakini bado hawakuweza kuiepusha timu yao na kipigo.

Portland Trail Blazers 126-118 Utah Jazz

Kwenye mchezo huu, MJ McCollum na Damian Lillard wameshirikiana vyema na kufanikiwa kufunga jumla ya vikapu 53 baina yao kwa upande wa Portland.

Naye Mitchell aliwaongoza Uttah kwa kufunga vikapu 27 peke yake licha ya timu yake kushindwa kuibuka na ushindi. Conley aliongeza vikapu 20 huku Rudy Gobert akifunga vikapu 13. 

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya