Pre-Season: Brooklyn Nets Wawatambia Lakers Kwenye Mchezo Wa Kutest Mitambo

13th October 2019

SHENZHEN, China- Brooklyn Nets wamewachapa Los Angeles Lakers kwa jumla ya vikapu 91-77 kwenye mchezo wa kujipima ubavu ili kujiweka sawa na msimu mpya wa ligi kuu ya mpira wa kikapu ya Marekani, NBA.

Brooklyn Nets
Brooklyn Nets
SUMMARY

Ligi ya NBA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 22, mwaka huu. Kwasasa ni kipindi cha kujiweka sawa ambapo timu zote zipo nchini China kwa ajili ya Pre season. 

Nyota kwa upande wa Nets alikuwa ni Carus LeVert ambaye amefanikiwa kufunga vikapu 22 ndani ya dakika 22 na kutoa assisti 5 kwenye mchezo huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo.

Taurean Prince hakuwa mbali ya LeVert kwani naye kwa upande wake amefanikiwa kufunga vikapu 14 kwenye mchezo huo.

Licha ya kupoteza mchezo huo lakini pia Lakers wanalo jambo la kuhofia baada ya kushuhidia nyota wao tegemezi Anthony Davis akipata majeraha wakati wa robo ya pili ya mchezo yaliyomlazimu kutolewa nje ya uwanja na kwenda kutibiwa.

Nao Nets walilazimika kumkosa Kyrie Irving ambaye aliumia tangu kwenye mchezo wa Alhamisi iliyopita.

Ligi ya NBA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 22, mwaka huu. Kwasasa ni kipindi cha kujiweka sawa ambapo timu zote zipo nchini China kwa ajili ya Pre season. 

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya