Patrick Aussems Amkingia Kifua Mwinyi Zahera

9th November 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania -Kocha wa Simba Patrick Aussems, ameshangazwa na uongozi wa watani zao Yanga kumtimua kocha Mwinyi Zahera.

Patrick Aussems
Patrick Aussems
SUMMARY

"Ni habari za kikatili sana walipaswa kumpa muda kwasababu timu asilimia kubwa inawachezaji wapya alihitaji kupewa muda ili kupata matokeo wanayo hitaji," amesema Aussems.

Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wake Dk. Mshindo Msolla,  siku ya Jumanne walitangaza kuachana na Zahera pamoja na benchi zima la ufundi.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Aussems amesema kuwa Yanga hawakumtendea haki Mkongomani huyo kwani alipaswa apewe muda wa kuijenga timu.

"Ni habari za kikatili sana walipaswa kumpa muda kwasababu timu asilimia kubwa inawachezaji wapya alihitaji kupewa muda ili kupata matokeo wanayo hitaji," amesema Aussems.

Alisema tangu Zahera aichukue Yanga timu imekuwa na mabadiliko makubwa kiuchezaji pamoja na changamoto inazopitia.

"Siwezi kuwazungumzia sana kwasababu mimi nimeajiriwa na Simba lakini kama mwanataaluma mwenzangu Yanga  hawakumtendea haki ni mtu aliyepambana kuipigania timu tangu alipoikabidhiwa na bado alikuwa anakuja vizuri kwasababu timu ni mpya lakini wameshindwa kumvumilia siyo sawa," amesema Aussems.

 Imeandaliwa na Raheem Mohamed