Paris Masters: Novak Djokovic Atinga Robo Fainali Baada Ya Kumfunga Kyle Edmund

1st November 2019

PARIS, Ufaransa- Mchezaji wa tenesi namba moja kwa ubora duniani, Novak Djokovic amefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Paris Masters baada ya kumfunga Klyle Edmund kwenye mchezo wa 16 bora.

Novak Djokovic
Novak Djokovic
SUMMARY

Hata hivyo licha ya kufungwa lakini hii ni wiki nzuri kwa Edmund ambaye kiwango chake ndani ya michuano hii kimempa nafasi ya kutajwa kwenye timu ya Uingereza itakayokwenda Madrid, Hispania kushiriki michuano ya Davis Cup.

Djokovic, 32, ameshinda kwa seti 7-6 (9-7) 6-1 na sasa atakutana na Stefanos Tsitsipas ambaye amemfunga Alex de Minaur kwa seti 6-3 6-4 kwenye mchezo mwingine.

Edmund, 24 ambaye alipoteza michezo 8 mfululizo kabla ya kushinda michezo miwili ndani ya michuano hii aliweza kumpa shida Djokovic ambaye ni bingwa mara nne kwenye seti za awali lakini alijikuta akizidiwa mwishoni na kupoteza mchezo.

Hata hivyo licha ya kufungwa lakini hii ni wiki nzuri kwa Edmund ambaye kiwango chake ndani ya michuano hii kimempa nafasi ya kutajwa kwenye timu ya Uingereza itakayokwenda Madrid, Hispania kushiriki michuano ya Davis Cup.

Kwengineko, Mbulgaria, Grigor Dimitrov ameonesha kiwango cha hali ya juu na kumfunga Dominic Thiem kwa seti 6-3 6-2 na sasa atakutana na Mchile, Cristian Garin.

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya