Ndondi: Mwakinyo Uso Kwa Uso na Mfilipino Novemba 29

15th October 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania -Bondia namba moja wa uzito wa kati Tanzania Hassani Mwakinyo, anatarajia kupanda ulingoni Novemba 29 mwaka huu kupambana na Arnel Tinampay kutoka Phillippines.

Hassan Mwakinyo
Hassan Mwakinyo
SUMMARY

"Huyu ndio Bondia namba moja nchini kwao Phillipines, ndio maana tukamchagua ili kumpa ushindani mzuri bondia wetu Mwakinyo kwani endapo atashinda anaweza kupandishwa uzani kutoka huu aliokuwa nao hivi sasa wa Kg 69 Super Walter Weight," amesema Msangi.

Mpambano huo wa raundi 10, umepangwa kufanyika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kuanzia saa 9 alasiri.

Akizungumza na SportPesa News, Mwakinyo amesema amejiandaa vyema kuhakikisha analiwakilisha taifa kwa kushinda pambano hilo ambalo anaamini litazidi kumpandisha.

"Nimefurahi kumpata Tinampay, kwasababu ni bondia mwenye rekodi kubwa kunizidi mimi lakini nitahakikisha nacheza kwa juhudi ili nishinde kwa ajili ya nchi yangu," alisema Mwakinyo.

Wadhamini njooni

Bondia huyo ambaye pia anashika namba moja kwa ubora Afrika kwa uzito wake, ameyaomba makampuni mbalimbali kujitokeza kumdhamini kama ilivyofanya kampuni ya SportPesa ili kumuongezea chachu ya kushinda pambano hilo.


Kwa upande wake Promota wa pambano hilo James Msangi, amesema wamemchagua Tinampay, kutokana na rekodi zake nzuri za kupigana mapambano 51 bila kupoteza kwa KO.

"Huyu ndio Bondia namba moja nchini kwao Phillipines, ndio maana tukamchagua ili kumpa ushindani mzuri bondia wetu Mwakinyo kwani endapo atashinda anaweza kupandishwa uzani kutoka huu aliokuwa nao hivi sasa wa Kg 69 Super Walter Weight," amesema Msangi.

Rekodi za Tinampay hajawahi kupoteza pambano kwa TKO, lakini pia anatajwa kushika nafasi ya bondia bora nchini mwake Man Packyao.

Milioni 100

Mwakinyo ambaye ni balozi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa, anatarajiwa kuchomoka na kitita cha zaidi ya Shilingi Milioni 100 pindi atakapopanda ulingoni

Imeandaliwa na Rahim Mohamed