Ndayiragije Mbioni Kupewa Kibarua Cha Moja Kwa Moja Kuinoa Taifa Stars

20th October 2019

DAR ES SALAAM, Tanzania- Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya taifa Etienne Ndayiragije, huenda akatangazwa kuwa Kocha Mkuu wa kudumu wa timu hiyo baada ya kukiongoza kikosi cha Stars kufuzu fainali za CHAN

Ettiene Ndayiragije
Ettiene Ndayiragije
SUMMARY

Ndayiragije aliteulikuwa kuwa kocha wa muda wa Stars,  baada ya kutimuliwa Mnigeria Emmanuel Amunike kufuatia matokeo mabaya kwenye michuano ya Afcon.

DAR ES SALAAM, Tanzania -Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya taifa Etienne Ndayiragije, huenda akatangazwa kuwa Kocha Mkuu wa kudumu wa timu hiyo  baada ya kukiongoza kikosi cha Stars kufuzu fainali za  CHAN pamoja na kucheza makundi kusaka tiketi ya fainali za kombe la dunia za Qatar 2022.

Imefahamika uongozi wa klabu ya Azam FC,  wakati wowote utatangaza kumrejesha aliyekuwa kocha wao Aristico Cioba kuchukua mikoba ya Ndayiragije.

Kocha huyo raia wa Burundi, amezungumza na SportPesa News, na kudai hajui chochote kuhusu taarifa hizo za kuondolewa Azam na kama itatokea hivyo atajua cha kuongea.

"Ninachofahamu bado nina mahusiano mazuri na waajiri wangu Azam na hata ruhusa ya kufanya kazi TFF, wao ndio wameniruhusu kwaiyo siwezi sema chochote hivi sasa," amesema Ndayiragije.

Inaelezwa kuwa makocha wasaidizi wa Taifa Stars Juma Mgunda, Selemani Matola na meneja Nadir Haroub 'Cannavaro'nao wanatarajiwa kupewa mikataba ya kudumu timu ya Taifa.

Ndayiragije aliteulikuwa kuwa kocha wa muda wa Stars,  baada ya kutimuliwa Mnigeria Emmanuel Amunike kufuatia matokeo mabaya kwenye michuano ya Afcon.

Akiwa kocha wa Stars Ndayiragije ameingoza timu hiyo kufuzu kupangwa hatua ya makundi ya kombe la Dunia kwa kuwatoa Burundi na pia fainali hizo za CHAN kwa kuwatoa Kenya na Sudan.


Imandaliwa na Rahim Mohamed