NBA: Philadelphia Waibuka Na Ushindi Huku Clippers Wakikwaa Kisiki

27th October 2019

PHILADELPHIA, Marekani- Nyota wa Philadelphia 76ers, Tobias Harris amefunga vikapu 29 na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa vikapu 117-111 dhidi ya timu ya Detroit Pistons.

Tobias Harris
Tobias Harris
SUMMARY

Kwenye mchezo huo tumeshuhuduia timu zote zikiwakosa wachezaji wake nyota. Kwa upande wa Philadelphia wao waliwakosa Joel Embiid akiwa na majeraha ya kifundo cha mguu huku Pistons wao wakimkosa mshambuliaji wao hatari Blake Griffin.

Mbali na Harris, Al Horford naye amechagiza ushindi huo kwa kiasi kikubwa akiwa amefunga vikapu 23 kwenye mchezo uliofanyika alfajiri ya leo.

Kwenye mchezo huo tumeshuhuduia timu zote zikiwakosa wachezaji wake nyota. Kwa upande wa Philadelphia wao waliwakosa Joel Embiid akiwa na majeraha ya kifundo cha mguu huku Pistons wao wakimkosa mshambuliaji wao hatari Blake Griffin.

Hata hivyo kukosekana kwa nyota hao hakukufanya mchezo huo kuwa mbaya kwani wachezaji waliopata nafasi walionesha uwezo wao na kuamsha shangwe kubwa kwa mashabiki waliolipa fedha zao kwa ajili ya kuangalia mechi hiyo.

Derrick Rose yeye alikuwa ni muhimili muhimu kwa Pistons na alifunga vikapu 31 ingawa havikutosha kuikoa timu yake na kipigo hicho kutoka kwa Philadelphia.

LA Clippers Wakwaa Kisiki

Devin Booker amefunga vikapu 30 na kufanya asissti 8 wakati akiisaidia timu yake ya Phoenix Suns kuibuka na ushindi wa kishindo wa vikapu 122-130 dhidi ya LA Clippers.

Clippers ambao wameanza ligi ya msimu huu kwa kishindo wakiwa wameshinda michezo yao miwili ya kwanza walijikuta katika wakati mgumu kukabiliana na nyota wadogo ambao walikuwa wanaonesha uwezo wa hali ya juu uwanjani.

Kelly Oubre Jr naye hakuwa mbali kufanya mambo yake baada ya kutupia vikapu 20 ikiwa ni kama sehemu ya kuchagiza ushindi huo dhidi ya timu ambayo inapewa nafasi ya kufanya vizuri msimu huu.

Nyota wa Clippers Kawhi Leonard yeye kwa upande wake alifunga vikapu 27 huku mastaa wawili Lou Williams na Montrezl Harrell wakifunga vikapu 51 kwa pamoja lakini bado haikutosha kuwa sababu ya wao kupata ushindi kwenye mchezo huo.

Matokeo mengine

Philadelphia 76ers 117-111 Detroit Pistons

LA Clippers 122-130 Phoenix Suns

Houston Rockets 126-123 New Orleans Pelicans

Miami Heat 131-126 Milwaukee Bucks (OT)

Toronto Raptors 108-84 Chicago Bulls

Boston Celtics 118-95 New York Knicks

Sacramento Kings 81-113 Utah Jazz

Orlando Magic 99-103 Atlanta Hawks

Indiana Pacers 99-110 Cleveland Cavaliers

Washington Wizards 122-124 San Antonio Spurs

Imeandaliwa na Badrudini Yahaya