NBA: Moto Wa Devin Booker Wapelekea Kipigo Cha Kwanza Kwa Philadelphia Msimu Huu

5th November 2019

PHILADELPHIA, Marekani- Nyota wa Phoenix Suns, Devin Booker amefunga alama 40 na kuisaidia timu ya kuibuka na ushindi wa vikapu 114-109 dhidi ya Philadelphia 76ers.

Devin Booker
Devin Booker
SUMMARY

Licha ya kufungwa lakini Al Horford alifunga vikapu 32 ikiwa ni vingi kwake msimu huu huku Tobias Harris akiongeza 24 na Furkan Korkmaz akifunga 20.

Hicho kinakuwa ni kipigo cha kwanza kwa Philadelphia msimu huu ambao waliuanza kwa kasi kubwa wakishinda michezo yao yote mitano ya awali waliyoshuka dimbani.

Mhispania, Ricky Rubio naye alifunga alama 21 kwenye mchezo huo huku Aron Baynes akifunga 15 na kelly Oubre akifunga alama 14 kwa upande wa Suns.

Ushindi huu ni wa tano kwa Suns ndani ya mechi saba walizocheza ikiwa ni rekodi nzuri inayolingana na ile ya msimu 2013-14 ambapo walifanya kama hivi.

Licha ya kufungwa lakini Al Horford alifunga vikapu 32 ikiwa ni vingi kwake msimu huu huku Tobias Harris akiongeza 24 na Furkan Korkmaz akifunga 20.

Philadelphia kwa mara nyingine tena leo wamecheza bila ya mshambuliaji wao nyota Joel Embiid aliyekuwa akimalizia adhabu ya kufungiwa mechi mbili baada kumsuguano uliotokea Jumatano iliyopita baina yake na mchezaji wa Minnesota Timberwolves, Karl Anthony Towns. 

James Harden Aandelea Kukiwasha

James Harden amefunga vikapu 44 na kufanya rebound 10 wakati akiiongoza timu yake ya Houston Rockets kwenye ushindi wa 107-100 dhidi ya Memphis Grizzlies.

Kwenye mchezo huo Harden amecheza bila ya pacha wake uwanjani Russell Westbrook ambaye amepumzishwa kwa mara ya kwanza msimu huu.

Matokeo Mengine:

Philadelphia 76ers 109-114 Phoenix Suns

Houston Rockets 107-100 Memphis Grizzlies

New Orleans Pelicans 125-135 Brooklyn Nets

Milwaukee Bucks 134-106 Minnesota Timberwolves

Portland Trail Blazers L-L Golden State Warriors

Detroit Pistons 99-115 Washington Wizards

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya