NBA: LeBron James Awasha Moto, Kobe Bryant Akishuhudia Jukwaani

18th November 2019

LOS ANGELES, Marekani- Mtaalamu Lebron James ameendeleza kiwango chake bora msimu huu baada ya alfajiri ya leo kufanikiwa kufunga alama 33 akiiwezesha timu yake ya LA Lakers kuibuka na ushindi wa 122-101 dhidi ya Atlanta Hawks.

Lebron James
Lebron James
SUMMARY

Mbali na kufunga alama hizo 33 ambazo zilikuwa ni nyingi ukilinganisha na wachezaji wengine kwenye mchezo huo lakini pia James alitoa pasi za kufunga 12.

Wakati James akifanya mambo hayo kwenye jukwaa alikwepo gwiji wa zamani wa Lakers, Kobe Bryant ambaye alikitumikia kikosi hicho tangu mwaka 1996 hadi alipotundika daluga mwaka 2016.

Mbali na kufunga alama hizo 33 ambazo zilikuwa ni nyingi ukilinganisha na wachezaji wengine kwenye mchezo huo lakini pia James alitoa asisti 12.

Kyle Kuzma naye aliongeza alama 17, Rajon Rondo 15 na mshambuliaji Anthony Davis yeye kwa upande wake alifunga alama 14 tu kwenye mchezo huo.

Kwa upande wa Hawks shujaa alikuwa ni Trae Young ambaye amefunga alama 31 na Cam Reddish alikuwa ni wa pili kwa upande wao akiwa na alama 13.

Celtic Wakalishwa Kibabe

Kwenye pambano ambalo lilikuwa ni kali na kusisimua liliwakutanisha Boston Celtic ambao walikuwa uwanjani dhidi ya Sacramento Kings.

Kwenye mpambano huo tumeshuhudia Celtic wakifungwa kwa jumla ya vikapu 100-99 na kusababisha kusitshwa kwa ile rekodi yao ya ushindi kwenye mechi 10 mfululizo msimu huu.

Buddy Hield ndiye aliyeongoza mauaji hayo akifunga alama 35 peke yake akiiongoza timu yake kushinda kwenye mchezo wa tano ndani ya mechi saba zilizopita.

Nemanja Bjelica aye alifunga alama 12 a rebound 14 huku Bogdan Bogdanovic akifunga alama 12 na asisti 10 kwenye mchezo huo.

Matokeo Mengine

Atlanta Hawks 101-122 LA Lakers

Boston Celtics 99-100 Sacramento Kings

Philadelphia 76ers 114-95 Cleveland Cavaliers

Denver Nuggets 131-114 Memphis Grizzlies

Washington Wizards 121-125 Orlando Magic

Golden State Warriors 100-108 New Orleans Pelicans

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya