NBA: LeBron James Awasha Moto Dhidi Ya Utah Jazz, Toronto Raptors Wakiangukia Pua

26th October 2019

LOS ANGELES, Marekani -LeBron James "The King" ameng'aa wakati akiisaidia timu yake ya LA Lakers kuibuka na ushindi wa 86-95 dhidi ya Uta Jazz.

Lebron James
Lebron James
SUMMARY

Kwenye mchezo huo tulishuhudia timu zikiwa zimeshikana kwa matokeo ya 43-43 dakika mbili tu baada ya kuanza kwa robo ya tatu lakini Lakers walipambana na kumaliza robo hiyo wakiwa mbele kwa vikapu 74-55.

Ushindi huo ni kwanza kwa LA Lakers msimu huu baada ya kuanza ligi kwa kipigo kutoka kwa majirani zao LA Clippers kwenye mchezo wa kwanza tu waufunguzi.

The King akiwa kwenye kiwango bora kabisa cha mchezo amefanikiwa kutundika vikapu 32 na kufanya assisti 10 kwa upande wa timu yake ambayo ilikuwa moto kwenye dimba la Staples Center.

Nyota mwingine wa timu hiyo ya Lakers, Anthony Davis naye alikuwa imara kuchagiza ushindi huo ambaye binafsi alifunga vikapu 21 huku akifanya block 5 na rebound 7.

Mlinzi wa kutumainiwa wa Lakers, Troy Daniels aliingia akitokea benchi na alifunga vikapu 15.

Kwa upande wao Utah, nyota alikuwa ni Donovan Mitchell ambaye amefunga vikapu 24 huku Mike Conley akifunga mara 13.

Mshambuliaji tegemezi wa Utah, Joe Ingles alikuwa na mchezo mgumu sana na alifanikisha kufunga vikapu 2 tu.

Utah pia walilazimika kucheza bila ya mshambuliaji wao mwingine Bojan Bogdanovic ambaye ali[ata majeruhi ya kifundo kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Thunder.

Kwenye mchezo huo tulishuhudia timu zikiwa zimeshikana kwa matokeo ya 43-43 dakika mbili tu baada ya kuanza kwa robo ya tatu lakini Lakers walipambana na kumaliza robo hiyo wakiwa mbele kwa vikapu 74-55.

Mabingwa Watetezi Wapigwa

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo ya mpira wa kikapu Toronto Raptors wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kupigwa kwa jumla ya vikapu 106-112 dhidi ya Boston Celtic.

Raptors walianza vizuri kwa kushinda mchezo wa kwanza lakini wamejikuta katika hali ya taharuki kwa kufungwa na Celtic ambao wao walifungwa kwenye mchezo wao wa kwanza wa msimu.

Jaylen Brown na Jayson Tatum kila mmoja alifunga vikapu 25 huku Kemba Walker akiongeza vingine 22 kwa upande wa Celtic.

Pascal Saikam amewaongoza Raptors kwa kufunga vikapu 33 huku Kyle Lowry akifunga 29 lakini hata hivyo pamoja na jitihada hizo lakini hawakuweza kuibuka na matokeo ya ushindi.

Matokeo Kamili

Utah Jazz 86-95 Los Angeles Lakers

Toronto Raptors 106-112 Boston Celtics

Minnesota Timberwolves 121-99 Charlotte Hornets

Phoenix Suns 107-108 Denver Nuggets (OT)

Dallas Mavericks 123-116 New Orleans Pelicans

New York Knicks 109-113 Brooklyn Nets

Portland Trail Blazers 122-112 Sacramento Kings

Chicago Bulls 110-102 Memphis Grizzlies

Washington Wizards 97-85 Oklahoma City Thunder

Imeandaliwa na Badrudin Yahayaa