NBA: LeBron James Awaongoza LA Lakers Kwenye Ushindi Wa Tano Mfululizo

4th November 2019

LOS Angeles, Marekani- LeBron Jemes ameendelea kuwa mwiba ndani ya kikosi cha LA Lakers akizidi kuwang'arisha na kufanikisha ushindi wa tano mfululizo baada ya kuwafunga San Antonio Spurs kwa jumla ya vikapu 103-96.

Lebron James
Lebron James
SUMMARY

Wakati Lakers wakifanya yao, majirani zao LA Clippers nao hawakuwa kimya bali nao walikuwa wanatoa adhabu kali kwa Utah Jazz baada ya kuwafunga kwa vikapu 94-105.

Mshambuliaji, Anthony Davis amefunga alama 25 huku akifanya rebound 11 kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na burudani ya kila aina kutoka kila upande.

James ama The King kama mashabiki wake wanavyopenda kumuita amefunga vikapu 21 kwenye mchezo huo, ametoa assisti 11 na amefanya rebound 13 kitu ambacho ni ngumu sana kuamini hasa ukiangalia umri wake ambao unakwenda maji ya jioni.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa The King kufanya hivyo. Baada ya kuanza msimu kwa kipigo kutoka kwa majirani zao LA Clippers, Lakers wamekuwa ni wa moto balaa wakishinda karibia kila mchezo.

Mafanikio ya kushinda mechi tano mfululizo hawakuyapata msimu uliopita licha ya kwamba walifanya vizuri.

LA Clippers Nao Wakanyaga

Wakati Lakers wakifanya yao, majirani zao LA Clippers nao hawakuwa kimya bali nao walikuwa wanatoa adhabu kali kwa Utah Jazz baada ya kuwafunga kwa vikapu 94-105.

Kama kawaida, Kawhi Leonard alikuwa mwiba kwa wapinzani akifunga alama 30 peke yake. Kwenye mchezo huo tulimshuhudia nyota huyo akianza taratibu sana na kufunga alama 5 tu kwenye kipindi cha kwanza.

Kurudi kwa kipindi cha pili ndipo makali ya Leonard yalipoamka na akafunga alama nyingine 25 na kumfanya amalize akiwa na alama 30 kwenye mchezo huo.

Matokeo mengine

LA Lakers 103-96 San Antonio Spurs

Utah Jazz 94-105 LA Clippers

Chicago Bulls 95-108 Indiana Pacers

Houston Rockets 100-129 Miami Heat

Dallas Mavericks 131-111 Cleveland Cavaliers

Sacramento Kings 113-92 New York Knicks

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya