NBA: LA Clippers Wapigwa Kwa Mara Ya Pili Mfululizo

15th November 2019

LOS ANGELES, Marekani- Timu ya LA Clippers wamekutana na kipigo cha vikapu 132-127 kutoka kwa New Orleans Pelicans.

NBA
NBA
SUMMARY

Jruwe Holiday amefunga alama 36 kwa wenyeji Pelicans na kuharibu siku ya Paul George ambaye leo ndiyo alikuwa anacheza mchezo wake wa kwanza ndani ya Clippers.

LOS ANGELES, Marekani- Timu ya LA Clippers wamekutana na kipigo cha vikapu 132-127 kutoka kwa New Orleans Pelicans.

Mchezo huo ni wa pili mfululizo kwa Clippers kufungwa ikiwa imepita siku moja tu tangu walipopoteza mchezo mbele ya Houston Rockets.

Jruwe Holiday amefunga alama 36 kwa wenyeji Pelicans na kuharibu siku ya Paul George ambaye leo ndiyo alikuwa anacheza mchezo wake wa kwanza ndani ya Clippers.

Frank Jackson naye aliongeza vikapu 23 kwenye ushindi huo huku Derrick Favors akifunga alama 20.

Lou Williams ndiye aliyekuwa nyota kwa upande wa Clippers akifunga vikapu 31 huku Rodney McGruder akifunga 20 na Montrezl Harrell akiongeza vyake 18.

Ni wazi kabisa Clippers ambao msimu huu wanapigiwa chapuo la kuwa mabingwa hawakuwa kwenye kiwango bora hasa mara baada ya kutoka kucheza na Rockets siku moja iliyopita.

Hadi timu zinakwenda mapumziko matokeo yalikuwa ni 72-59 lakini Clippers wakapunguza gape hilo na kufikia tofauti ya nne wakati George akifunga alama 7 kwenye 11 za mwanzo.

Matokeo Mengine

LA Clippers 127-132 New Orleans Pelicans

Dallas Mavericks 103-106 New York Knicks

Chicago Bulls 115-124 Milwaukee Bucks

Atlanta Hawks 112-128 Phoenix Suns

Miami Heat 108-97 Cleveland Cavaliers

Brooklyn Nets 93-101 Denver Nuggets

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya