NBA: LA Clippers Wachomoza Na Ushindi Wa Jioni Mbele Ya Houston Rockets

23rd November 2019

LOS ANGELES, Marekani- Kawhi Leonard amepigilia misumari ya sekunde za mwisho na kuihakikishia timu yake ya LA Clippers ushindi wa vikapu 122-119 dhidi ya Houston Rockets kwenye mchezo ambao ulikuwa na vuta ni kuvute ya aina yake.

Houston Rockets
Houston Rockets
SUMMARY

Zikiwa zimesalia sekunde 30.8 mchezo kuisha Rockets walikuwa wanaongoza kwa vikapu 117-115. Hata hivyo Williams alifunga alama 3 na kufanya ubao wa matokeo kubadilika na sasa Clippers wakawa wanaongoza kwa 118-117.

Lou Willims ndiye aliyefunga alama nyingi kwa upande wa Clippers akifunga vikapu 26 vyote akivifunga kwenye kipindi cha pili.

Leonard yeye alimaliza mchezo akiwa na alama 24 lakini ndiyo unaweza kusema kuwa aliibuka nyota wa mchezo akifunga pointi za ushindi kwenye sekunde 15 za mwisho kabla ya mchezo kuisha na kupelekea ushindi wanne mfululizo kwa timu yake.

James Harden licha ya kufunga vikapu 37 kwa upande wa Rockets lakini bado mambo yalikuwa magumu kwa upande wao na hadi kupelekea kushindwa kuibuka na ushindi.

Russell Westbrook naye aliongeza alama 22 kwa Rockets huku Clint Capela akifunga 17 na rebound 19.

Zikiwa zimesalia sekunde 30.8 mchezo kuisha Rockets walikuwa wanaongoza kwa vikapu 117-115. Hata hivyo Williams alifunga alama 3 na kufanya ubao wa matokeo kubadilika na sasa Clippers wakawa wanaongoza kwa 118-117.

Watu wakiamini mchezo unaelkea kuisha kwa Clippers kuibuka na ushindi huo, Harden alifunga alama mbili za haraka zikiwa zimesalia sekunde 22 na kuwafanya Rocktes kuwa mbele kwa alama 119-118.

Zikiwa zimesalia sekunde 15, Leonard alifunga alama mbili na Paul George akaiongeza nyingine mbili huku mchezo ukiwa umebakia sekunde 1.2 na hivyo kukamilisha ushindi huo wa machozi, jasho na damu.

Matokeo Mengine

Houston Rockets 119-122 LA Clippers

Los Angeles Lakers 130-127 Oklahoma City Thunder

Boston Celtics 92-96 Denver Nuggets

Cleveland Cavaliers 101-143 Dallas Mavericks

San Antonio Spurs 104-115 Philadelphia 76ers

Miami Heat 116-108 Chicago Bulls

Sacramento Kings 97-116 Brooklyn Nets

Golden State Warriors 109-113 Utah Jazz

Atlanta Hawks 102-128 Detroit Pistons

Charlotte Hornets 118-125 Washington Wizards

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya