NBA: Kyle Kuzma Aing'arisha LA Lakers Dhidi Ya Suns Akitokea Benchi

13th November 2019

LOS ANGELES, Marekani -Kyle Kuzma ameibuka shujaa wa timu ya LA Lakers baada ya kufunga alama 23 akitokea benchi na kuisadia timu yake kupata ushindi wa jioni wa vikapu 123-115 dhidi ya Phoenix Suns.

Le bron James
Le bron James
SUMMARY

Kabla ya kupoteza mchezo dhidi ya Raptors, timu ya Lakers ilikuwa na mtiririko mzuri wa wimbi la matokeo ya ushindi ambapo walishinda mara saba mfululizo.

LOS ANGELES, Marekani -Kyle Kuzma ameibuka shujaa wa timu ya LA Lakers baada ya kufunga alama 23 akitokea benchi na kuisadia timu yake kupata ushindi wa jioni wa vikapu 123-115 dhidi ya Phoenix Suns.

Wachezaji wengine waliochangia kwa nguvu ushindi huo ni pamoja na Athony Davis aliyefunga vikapu 24 huku LeBron James "The King" akifunga vikapu vyake 19 pamoja na asisti 11.

Ricky Rubio amefunga vikapu 21 na asisti 10, Devin Booker naye akifunga vikapu 21 huku Aron Baynes akufunga 20 kwa upande wa timu ya Suns.

Ushindi huu umekuja siku mbili tangu Lakers walipopoteza mchezo wao dhidi ya mabingwa watetezi Toronto Raptors.

Kabla ya kupoteza mchezo dhidi ya Raptors, timu ya Lakers ilikuwa na mtiririko mzuri wa wimbi la matokeo ya ushindi ambapo walishinda mara saba mfululizo.

Ushindi huo ulianzia kwenye mechi ya pili ya msimu ikiwa ni siku chache tangu walipopokea kichapo kutoka kwa majirani zao LA Clippers kwenye mechi ya ufunguzi.

Kwa kifupi ni kwamba kwenye mechi kumi walizoshuka uwanjani hadi hivi sasa, Lakers wameshinda mechi 8 na wamefungwa mechi 2.

Wachezaji ambao wamekuwa moto sana katika kufanikisha mafanikio hayo ni Davis ambaye anashirikiana vizuri sana na Lebron.

Matokeo Mengine:

Los Angeles Lakers 123-115 Phoenix Suns

Brooklyn Nxets 114-119 Utah Jazz

Cleveland Cavaliers 97-98 Philadelphia 76ers

Atlanta Hawks 125-121 Denver Nuggets

New York Knicks 102-120 Chicago Bulls

Detroit Pistons 108-117 Miami Heat

Oklahoma City Thunder 85-111 Indiana Pacers

Portland Trail Blazers 99-107 Sacramento Kings

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya