NBA: Kemba Walker Aiongoza Celtic Kushinda Mechi Ya 8 Mfululizo

12th November 2019

BOSTON, Marekani -Kemba Walker amefunga vikapu 29 na kuiwezesha timu yake ya Boston Celtic kuibuka na ushindi 116-106 dhidi ya Dallas Mavericks.

NBA
NBA
SUMMARY

Kwenye mchezo mwingine tumemshuhudia Kawhi Leonard akirudi nyumbani na kuwa sehemu ya kufanikisha ushindi kwa timu yake ya LA Clippers dhidi ya waajiri wake wa zamani Toronto Raptors ambao ni mabingwa watetezi.

BOSTON, Marekani -Kemba Walker amefunga vikapu 29 na kuiwezesha timu yake ya Boston Celtic kuibuka na ushindi 116-106 dhidi ya Dallas Mavericks.

Ushindi huo ni wa nane mfululizo kwa timu ya Boston Celtic ambao kwasasa wapo kwenye kiwango bora sana.

Jaylen Brown naye alifunga vikapu 25 kwenye mchezo huo na akafanya rebound 11 huku Marcus Smart akiongeza alama nyingine 17.

Kwenye mchezo huo, Boston walicheza kwa mara ya kwanza bila ya mshambuliaji wao hatari Gordon Hayward ambaye anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki sita baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye mkono wake wa kushoto.

Luka Doncic alifunga vikapu 34 ambavyo ni vingi zaidi kwenye mchezo huo lakini bado hakuiwesha timu yake kuipuka kipigo cha tano mfululizo ugenini.

Kawi Leonard Arudi Nyumbani

Kwenye mchezo mwingine tumemshuhudia Kawhi Leonard akirudi nyumbani na kuwa sehemu ya kufanikisha ushindi kwa timu yake ya LA Clippers dhidi ya waajiri wake wa zamani Toronto Raptors ambao ni mabingwa watetezi.

Kawhi alikwepo Raptors msimu uliopita ambapo alisaidia timu hiyo kupata taji kwa mara ya kwanza na baada ya kumalizika kwa msimu alijiunga na Clippers.

Tangu kujiunga na Clippers ameifanya timu hiyo kuwa moja kati ya timu tishio ndani ya ligi tangu michuano hiyo ilipoanza Oktoba 22.

Kwenye mchezo wa leo Kawhi amefunga alama 12 na kuiwezesha timu yake hiyo mpya ya Clippers kushinda kwa 98-88 dhidi ya Raptors.

Low Williams ndiye aliyekuwa nyota zaidi kwa upande wa Clippers akifunga alama 21 akitokea kwenye benchi. Montrezl Harrell anaye alifunga 14 kwenye ushindi huo.

Pascal Siakam ameendelea kuwa na balaa zito ndani ya jezi za Raptors baada ya kufunga alama 16 pia kufanya asisti 6 na rebound 10. Hata hivyo bado hakuinusuru timu yake na kipigo.

Matokeo Mengine:

Dallas Mavericks 106-116 Boston Celtics

Toronto Raptors 88–98 LA Clippers

Houston Rockets 122-116 New Orleans Pelicans

Memphis Grizzlies 113-109 San Antonio Spurs

Minnesota Timberwolves 120-114 Detroit Pistons

Utah Jazz 122–108 Golden State Warriors

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya