NBA: Kawhi Leonard Awasha Moto, Clippers Wakiisambaratisha Spurs 103-97

1st November 2019

LOS ANGELES, Marekani- Kawhi Leonard amefunga alama 38 na rebound 12 wakati akiisaidia timu yake ya LA Clippers kuipa kipigo cha vikapu 103-97 dhidi ya San Antonio Spurs.

Kawhi Leonard
Kawhi Leonard
SUMMARY

DeMar DeRozan amefunga alama 29, Derrick White naye akafunga alama 20 akitokea benchi huku Rudy Gay akiongeza alama 12 na rebound 9 kwa upande wa Spurs.

Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Spurs ambao walianza kwa ushindi ndani ya mechi zao tatu za awali.

Montrezl Harrell naye amefunga alama 24 akitokea benchi huku Lou Williams akiongeza alama zake 12 kwa upande wa Clippers.

DeMar DeRozan amefunga alama 29, Derrick White naye akafunga alama 20 akitokea benchi huku Rudy Gay akiongeza alama 12 na rebound 9 kwa upande wa Spurs.

Mechi hiyo imekuwa ni ya tatu baina Leonard na DeRozan kukutana tangu Spurs walipomuuza Leonard kwenda Toronto Raptors, Julai, 2018 kwenye dili ambalo tulishuhudia DeRozan akijiunga Spurs kama sehemu ya makubaliano.

Leonard alikwenda na kuiongoza Raptors kwenye taji la kwanza la NBA, kisha Julai, mwaka huu akasaini mkataba wa miaka mitatu na Clippers wenye thamani ya dola milioni 103.

Matokeo Kamili:

San Antonio Spurs 97-103 LA Clippers

Denver Nuggets 107-122 New Orleans Pelicans

Miami Heat 106-97 Atlanta Hawks

Imeandaliwa na Badrudin Yahaya